Header Ads Widget

WANANCHI SHINYANGA WAMEASWA KUTUNZA MAZINGIRA, KULINDA VIVUTIO VYA UTALII

 
Afisa Maliasili na uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga

Na Halima Khoya, SHINYANGA

WANANCHI wa Manispaa ya Shinyanga, wameaswa kutunza Mazingira ili kuendelea kulinda vivutio vya utalii.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa Maliasili na uhifadhi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema utunzaji wa mazingira utasaidia kuimarisha vivutio vya utalii wa ndani, hali ambayo itasaidia kuongeza mapato ya ndani na kukuza uchumi wa Taifa.

“Uharibifu wa Mazingira ni kikwazo kikubwa cha kudumaza utalii wa ndani na kuikosesha nchi mapato,”amesema Manjerenga.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga wajitokeze kwa wingi siku ya uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour awamu ya pili, ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Julai 30 mwaka huu, itakayo ambatana na utambulisho wa vivutio vya utalii ndani ya Manispaa ya Shinyanga, kikiwamo kisima cha maji ya moto Ibadakuli.

Post a Comment

0 Comments