Header Ads Widget

RC MJEMA ATAKA UZALENDO ZOEZI LA KUHESABIWA SENSA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa , ambao watakwenda kufundisha Makarani wa Sensa ngazi ya wilaya.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewataka Makarani wa zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na makazi, kutanguliza uzalendo kwenye zoezi hilo, ili lifanikiwe kwa asilimia 100.

Mjema amebainisha hayo leo Julai 25, 2022 wakati akifunga mafunzo ya wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa, ambao nao watakwenda kutoa mafunzo kwa Makarani wa Sensa ngazi ya wilaya.

Amesema kwenye zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi tayari baadhi ya watu wameshaanza kupotosha zoezi hilo, kuwa ni kuleta kodi ya kichwa, na kuwataka Makarani wa Sensa wasiwe nao sehemu ya upotoshaji wa zoezi hilo bali wawe waelimishaji juu ya umuhimu wa kuhesabiwa Sensa.

“Katika zoezi hili la kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi nawaomba Makarani mtangulize uzalendo, muwe waadilifu, na kufanya kazi kwa bidii,kwa sababu Serikali na Taifa kwa ujumla linawategemea ninyi,”amesema Mjema.

Aidha, amewataka pia viongozi ajenda yao kwenye mikutano mbalimbali elimu ya Sensa iwepo hadi siku ya zoezi hilo Agosti 23 mwaka huu, na kuondoa upotoshaji uliopo kuwa Sensa ni kuleta kodi ya kichwa, jambo ambalo siyo la kweli.

Amesema lengo la Sensa ya watu na Makazi ni Serikali kutaka kupata idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo, ili iwe rahisi kupanga mikakati yake ya maendeleo kwa wananchi, na kuwatekelezea kwa uwiano sawa na si vinginevyo.

Pia amewataka wahitimu wa Mafunzo ya Sensa ngazi ya Mkoa, wakawafundishe vizuri Makarani ngazi ya wilaya na wasimamizi wa zoezi hilo la Sensa ili lifanikiwe kwa asilimia 100 na Serikali kupata takwimu sahihi ya idadi ya watu wake kwa kila eneo.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa mkoani Shinyanga Eliud Kamendu, alisema Mafunzo hayo ya wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa yamechukua muda wa siku 21 na jumla ya washiriki ni 194 .

Alisema Mafunzo yalianza kutolewa kwa kufundisha Dodoso la jamii, Makundi Maalumu, Majengo, na yalikuwa yakitolewa kwa nadharia na vitendo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa , ambao watakwenda kufundisha Makarani wa Sensa ngazi ya wilaya.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa , ambao watakwenda kufundisha Makarani wa Sensa ngazi ya wilaya.

Mratibu wa Sensa mkoani Shinyanga Eliud Kamendu, akitoa taarifa ya mafunzo hayo ya wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa.

Wahitimu wa mafunzo ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Mkoa wakiwa ukumbini, ambao watakwenda kufundisha Makarani wa Sensa ngazi ya wilaya.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kulia) akimkabidhi Zawadi ya Cheti na Pesa Mhitimu wa mafunzo ya Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Mkoa ambaye ni miongoni mwa waliofanya vizuri kwenye mafunzo hayo Mariam Mohamed.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiendelea kutoa Zawadi kwa Wahitimu waliofanya vizuri

Zawadi zikiendelea kutolewa.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa, ambao watakwenda kufundisha Makarani wa Sensa ngazi ya wilaya.

Na Marco Maduhu, Halima Khoya SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments