Header Ads Widget

DAKTARI ADAKWA TUHUMA KUMFANYIA NGONO YA MDOMONI MJAMZITO WAKATI WA UPASUAJI


Daktari wa ganzi alikamatwa mapema Jumatatu asubuhi baada ya kushtakiwa kwa kumbaka mgonjwa aliyelazwa wakati wa upasuaji katika Hospitali ya Wanawake ya Heloneida Studart huko Rio de Janeiro.

Kwa mujibu wa Polisi, mwanamume huyo alinaswa na ujumbe wa usaidizi wa Wanawake wa jiji hilo, baada ya uhalifu huo kurekodiwa kwenye video.

Maafisa wa polisi walikimbilia katika kituo hicho baada ya maafisa wa kitengo cha afya ambao walikuwa wakihofia utendaji wa daktari huyo wa ganzi na kumpiga picha wakati wa upasuaji.

Daktari huyo alitambuliwa na mamlaka kuwa Giovanni Quintella Bezerra.

Kulingana na kitengo cha Habari kilichofanikiwa kupata kanda hiyo ya video wakati wa tukio la uhalifu , mtu huyo aliingiza uume wake katika kinywa cha mwanamke huyo wakati alipokuwa katika ganzi.

Polisi walisema kwamba Quintella Bezerra alituhumiwa kwa tukio la ubakaji dhidi ya mtu ambaye alikuwa hawezi kujitetea. Anakabiliwa na kifungo jela cha kati ya miaka 8 hadi 15.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO BBC SWAHILI.


Post a Comment

0 Comments