Header Ads Widget

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DK. CHANA AVUTIWA NA TAMASHA LA UTAMADUNI MKOANI SHINYANGA, AZINDUA FILAMU YA ROYAL TOUR

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana, akipiga Ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana, ameeleza kuvutiwa na Tamasha la utamaduni mkoani Shinyanga, ambalo linafundisha mambo mbalimbali ya mila na desturi kwa wananchi na hasa watoto wa kizazi kipya, pamoja na kuzindua Rasmi Filamu ya Royal Tour mkoani humo.

Waziri Chana amebainisha hayo leo June 6,2022 wakati akizundua Tamasha la utamaduni mkoani Shinyanga, akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuwa amefurahishwa kuona mkoani huo unaunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani za kutangaza masuala ya utalii na tamaduni hapa nchini.

Amesema Matamasha ya utamaduni ni mazuri sababu yanafaida ya kuendeleza umoja, upendo na mshikamano, kwa watu kujifunza namna ya kuishi kwa umoja pamoja na watoto kufundishwa maadili mema.

“Nimefurahishwa na Tamasha hili la utamaduni hapa Shinyanga, mmeonyesha mfano mzuri, na nina agiza kwa Mikoa yote hapa nchini ifanye Matamasha kama haya ya utamaduni na kuonyesha historia zake,”amesema Dk. Chana.

“Matamasha haya ya utamaduni ni mazuri sababu yanafundisha pia watoto wetu kufahamu lugha za asili na namna ya kuishi katika maadili mema, na kutoathiriwa na ulimwengu wa utandawazi, bali watumie mitandao ya kijamii kupata maarifa na uzalishaji mali,”ameongeza.

Aidha, amewataka pia Machief wa Kabila la Kisukuma wamuunge mkono Chief mwenzao Rais Samia Suluhu Hassani (Hangaya), kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Agost 23 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Waziri Chana amekemea vitendo vya kiovu na ukatili ambavyo vinatendeka ndani ya jamii, na kuwaomba Machief waisaidie Serikali kumaliza vitendo hivyo, ili wananchi waishi kwa amani na upendo kwa kuenzi maisha ya ma-babu.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Machifu Tanzania Nyamilonda Mikomangwa, amesema ana mpongeza Rais Samia kwa kutengeneza Filamu ya Royal Tour ambayo imetangaza mambo ya utalii na utamaduni hapa nchini na kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi.

Chifu Mikomangwa amesema wameahidi pia Rais Samia kumuunga mkono kwenye Suala la Sensa ya watu na makazi, kwa kuelimisha jamii katika himaya zao za kimila na wananchi wote kwa ujumla, ili washiriki zoezi hilo kimamilifu na kuirahisishia Serikali katika mipango yake ya maendeleo kwa wananchi wake.

Naye Mwenyekiti wa Machifu mkoani Shinyanga Charles Njange (Chidola), ameiomba Serikali mkoani humo, kuboresha miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami kwenye maeneo ya vivutio ili kufikike kwa urahisi, pamoja na kukarabati Ikulu ambazo zimeshakuwa mapango ili zibakiwa kuwa sehemu za makumbusho na watu kutalii katika maeneo hayo na kujifunza vitu vya kale.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesema wameandaa Tamasha hilo la utamaduni, ili kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassani katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania, na kutangaza utalii wa ndani kupitia vivutio vya kitamaduni vilivyopo mkoani Shinyanga.

Amesema Tamasha hilo la utamaduni mkoani Shinyanga litakuwa endelevu, ambapo wananchi wa Mkoa huo wa Shinyanga watakuwa wakifika kwenye kijiji hicho cha utamaduni, ambacho kimetengenezwa katika eneo la Butulwa Oldshinyanga kujifunza mambo mbalimbali ya mila na desturi za kabila lao.

Kauli Mbiu ya Tamasha hilo la utamaduni mkoani Shinyanga inasema “Utamaduni wetu, Urithi wetu, Jiandae kuhesabiwa.”

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana, akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye Tamasha la Utamadani mkoani humo.

Katibu Mkuu umoja wa Machief Tanzania Nyamilonda Mikomangwa akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa Machifu mkoani Shinyanga Charles Njange (Chidola) akizungumza kwenye Tamasha la Utalii mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto), akiwa na Mkuu wa Kishapu Joseph Mkude (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Machifu wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Wananchi wakiwa kwenye Tamasha la Utamadani mkoani Shinyanga.

Machifu wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Tamasha la Utamaduni likiendelea.

Wananchi wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni.

Wananchi wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk, Pindi Chana akikata utepe kuzindua Rasmi Tamasha la Utamaduni na Kijiji cha Utamaduni mkoani Shinyanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk, Pindi Chana, akipiga Ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk, Pindi Chana, akiendelea kupiga Ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk, Pindi Chana (kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, wakitwanga Nafaka kwa kutumia kinu kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana, akipokea zawadi ya Chungu na Jiko la udongo la kitamaduni, kutoka kwa Machifu, (kushoto) ni Chifu Nshoma Haiwa kutoka Kahama na kulia ni Chifu Nyaso Fundikila Skonge Vijijini.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk, Pindi Chana, akiendelea kupokea Zawadi za kitamaduni.

Hamisi Mgeja, katikati akiwa na baadhi ya viongozi kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Tamasha la Utamaduni likiendelea mkoani Shinyanga.

Monekano wa kijiji cha Utamaduni mkoani Shinyanga.

Muonekano wa Kitanda cha kulalia Mtemi, ambacho kipo ndani ya nyumba katika kijiji cha Utamaduni mkoani Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wakiangalia masuala ya Utamaduni katika kijiji cha Utamadauni.

Masuala ya Utamaduni yakiendelea.

Masuala ya Utamaduni yakiendelea.

Buruduni mbalimbali zikiendelea kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Buruduni mbalimbali zikiendelea kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Buruduni mbalimbali zikiendelea kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Wanyama aina ya Fisi wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Wanyama wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoani Shinyanga.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Pindi Chana awali akiwasili kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Post a Comment

0 Comments