Header Ads Widget

SHAHIDI AANGUA KILIO MAHAKAMANI AKIMTAMBUA MUUAJI WA MUMEWE

   

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza iliyoketi Geita, jana iliahirishwa mahakama kwa muda baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mke wa marehemu, Samwel Songoma, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliopora fedha zake.
Shahidi huyo ambaye ni wa nne kwa upande wa mashtaka, alitolewa nje ya mahakama kwa muda baada ya kuangua kilio alipotakiwa kumtambua mtu aliyemuua mume wake.

Mshtakiwa katika kesi hiyo ni Daniani Adrea, maarufu Kamkono.

Mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani mbele ya Jaji Lilian Itemba na aliposomewa shtaka lake alikana kuhusika na kosa la mauaji ya Samwel Songoma kwa kumpiga risasi tumboni.

Upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Janeth Kisibo, ambaye alisema atakuwa na mashahidi watatu na yuko tayari kuwasikiliza.

SOMA ZAIDI HAPA-chanzo Nipashe

Post a Comment

0 Comments