Header Ads Widget

SABABU KESI YA SABAYA KUAHIRISHWA


Uvimbe uliopo kichwani mwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ambapo anatakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji.

 Mawakili wa upande wa utetezi kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuahirisha kesi hiyo ili Sabaya apelekwe hospitali kutibiwa kutokana na uvimbe alionao kichwani.

Akitoa ombi hilo leo Jumanne Juni 7, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salome Mshasha, Wakili Hellen Mahuna amesema mshitakiwa namba moja ambaye ni Sabaya ni mgonjwa hivyo anapaswa kwenda kufanyiwa upasuaji.

"Mshitakiwa namba moja ni mgonjwa kutokana na uvimbe uliopo kichwani alioupata akiwa kazini, hivyo tunaomba kesi hii iahirishwe ili akafanyiwe upasuaji," amesema Wakili Mahuna

Wakili wa upande wa mashtaka,Verediana Mlenzi ameileza mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI

Post a Comment

0 Comments