Header Ads Widget

WAZIRI MKUU MAJALIWA AELEZA BOHARI KUU YA DAWA 'MSD' ILIVYOPIGA FEDHA ZA UVIKO-19

Majaliwa aeleza namna fedha za Uviko-19 zilivyopigwa MSD


 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini (PSPTB) kuwachukulia hatua za kinidhamu waliohusika na ubadhirifu kwenye manunuzi ya vifaa vya afya katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ambavyo vilipaswa kununuliwa kwa fedha za Uviko-19.

Pia, Majaliwa ameagiza Bodi hiyo kufika MSD Jumatatu Mei 9, 2022 kwa ajili ya kuanza kuwahoji waliohusika na ununuzi huo ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Majaliwa ametoa maagizo hayo yasema hao leo Mei 5,2022 katika uzinduzi wa wiki ya ununuzi wa umma iliyoratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na taasisi za ununuzi na ugavi ambazo ni PPRA,PPAA, PSPTF na GPSA jijini Arusha.

Amesema kuwa fedha hizo zilipaswa kununua vifaa hivyo ambavyo vingesambazwa katika hospitali za mikoa, wilaya zanahati na vituo vya afya kote nchini huku akionyesha namna ambavyo manunuzi yalivyofanya.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments