Header Ads Widget

TANCCOOPS WAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA, WALIA NA VIONGOZI MAMLUKI KUCHAFUA USHIRIKA


Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vikuu vya ushirika Tanzania (TANCCOOPS) na zao la Pamba Zainab Mahenge akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKISHO la vyama vikuu vya ushirika Tanzania (TANCCOOPS) ambavyo vinajishughulisha na kilimo cha zao la Pamba, wamefanya mkutano Mkuu wa pili wa mwaka, huku wakilia na baadhi ya viongozi ambao wamedai ni Mamluki, na wapo kwa ajili ya kuchafua ushirika.


Mkutano huo wa (TANCCOPS) umefanyika leo Mei 5, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU).

Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo Kwiyolecha Nkilijiwa, ambaye ni Mwenyekiti wa (SHIRECU), alisema vyama vya ushirika vimekuwa vikichafuliwa na baadhi ya viongozi ambao hawapo kwa ridhaa ya vyama hivyo (Mamluki) wakiwamo watendaji na wenyeviti, bali wapo kwa ajili ya kuchafua ushirika.

"Vyama vya ushirika tunachafuliwa na viongozi mamluki wakiwamo watendaji na wenyeviti, wamechomekwa humu kwa ajili ya kuchafua ushirika, na ili tuwesafi tunapaswa kuwaondoa" alisema Nkilijiwa.

Aidha, alisema katika mipango mingi ambayo inapangwa kujenga ushirika, wao wamekuwa wakitoa siri kwa mabosi wao ili kuangusha ushirika, kwa sababu baadhi yao wanatoka kwenye makapuni binafsi ya ununuzi wa Pamba na wamechomekwa kwa kazi hiyo.

"Hapa Mrajisi msaidizi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga, ametuambia vyama vya ushirika tuingie sasa kwenye ushindani wa kibiashara, lakini utashangaa yote tulivyozungumza humu yanafika huko na kuvuruga mikakati yote ya kuinua vyama vya ushirika," aliongeza Nkilijiwa.

Kwa upande wake Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace, akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vyama vya ushirika vinapaswa kuanza kujiendesha kibiashara, ili viinuke na kumkomboa mkulima wa zao la Pamba kiuchum.

"Vyama vya Ushirika inatakiwa ifike mahali vijiendeshe kibiashara, Ushirika ni sawa na Private sector, zalisheni mbegu na kuziuza, shindaneni kibiashara," alisema Boniphace.

Katika hatua nyingine aliwataka wajumbe wa vyama vya Ushirika wanapokuwa wakichagua viongozi, wachague wale wenye uwezo, na siyo kuchagua viongozi kwa Rushwa, kujuana, na kishabiki, ili kuepuka kupata viongozi wasio wachapakazi.

Naye Grace Mwagembe ambaye ni Mrajisi msaidizi kutoka Tume ya maendeleo ya Ushirika, aliwataka viongozi wa vyama vya ushirika kuwa wabunifu kwa sababu ushirika ni biashara, pamoja kuweka mikakati ya kuwapatia wakulima pembejeo kwa muda muafaka.
Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vikuu vya ushirika Tanzania (TANCCOOPS)vinavyojishughukisha na zao la Pamba Zainab Mahenge akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho Kwiyolecha Nkilijiwa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) akizungumza kwenye mkutano huo.

Mrajisi msaidizi kutoka tume ya maendeleo ya ushirika makao makuu Dodoma Grace Mwagembe akizungumza kwenye mkutano huo.

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Shinyanga Hilda Boniphace akizungumza kwenye mkutano huo.

wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments