Header Ads Widget

SHIRIKA LA THUBUTU LAZINDUA MRADI WA KUHAMASISHA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZAO WENYEWE BILA KUTEGEMEA NGUVU YA SERIKALI

Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Afrika Initiatives Jonathan Manyama akizungumza wakati wa uiznduzi wa mradi huo

Na Estomine Henry, SHINYANGA.

Mradi wa Hisani katika jamii( Community philanthropy) wa kuchochea na kuhamasisha jamii kuhusika katika kutatua changamoto zao bila kutegemea nguvu ya Serikali na Ruzuku za wadau katika kuleta maendeleo, umezinduliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Thubutu Africa Initiatives (TAI) katika manispaa ya Shinyanga.

Mradhi huo wa Hisani katika jamii( community philanthropy) umezinduliwa Ijumaa Mei 20,2022 katika hoteli ya vigmark
  na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga aliyewakilishwa na Chila Mosesi ambaye ni Afisa Mipango na Mratibu kutoka Mkoa wa Shinyaga na kuhudhuliwa na watendaji wa kata,maafisa maendeleo ,wadau kutoka asasi za kiraia,waandishi wa habari na wenyeviti wa mitaa kutoka kata za oldshinyanga,mjini,lubaga na mwamalili ambapo mradi huo utatekelezwa. 
 
 Mosesi akizungumza kwenye kikao hicho amesema kuwa ni jambo la fursa kubwa hasa kwa viongozi ndani ya jamii kuweza kutafuta mbinu za kutatua changamoto za jamii kupitia wadau.
 
" Ni jambo la furaha kwetu sote kuona tunakwenda kutatua changamoto kwa jamii kupitia rasilimali tulizonanzo katika jamii yetu bila kisubili fedha za serikali na wadau wa maendeleo"Amesema Mosesi.

Naye Mkurugenzi wa Shirila la Thubutu Africa Initiatives ( TAI) Jonathan Manyama amesema utamaduni huu wa kuchangia maendeleo umekuwepo ila haujawekwa katika mfumo rasmi wa kuweza kuwa wa muda mrefu au mfupi kwa kuwekeza kufatiliwa na kusimamiwa vizuri katika jamii ili kutatua changamoto zilizopo.

" Mfumo huu umekuwa ukitumika nchi zingine na kuleta maendeleo kwa jamii bila kusubili ruzuku za wahisani wa maendelo na fedha za serikali, Ni suala la jamii kubadili mitizamo kwa kujitolea zaidi kuhusu maendelo yanayowazunguka" Amesema Jonathan

Akiongeza Jonathan Manyama amesema ,serikali inapata mzigo kwa kuwa haikuwanda watu wake kwa muda mrefu kuhusu kujitolea kwa ajili ya maendelo yao.

Naye kwa upande wake,Mkurugenzi shirika la TVMC na mjumbe wa baraza la Taifa NGO(NACONGO) kutoka Shinyanga ,Mussa Ngangala amesema huu ni uwekezaji ndani ya jamii husika na una ifanya jamii kutumia rasilimali zake kwa ajili ya maendeleo yake.

" Huko nyuma niliwahi kujitolea kutengeneza barabara ya mtaa wangu wa kitangili kwa kuleta greda ila wananchi waliniambi niache kihelehele na wakasema hilo ni suala la serikali,Ki ukweli jamii ina mtazamo wa kusubili serikali katika mambo mengi.

Aidha, Diwani wa kata ya Lubaga ,Reuben Dotto alishukuru kwa mradi huo kuanza kutekelezaa katika kata yake na aliahidi kuhakikisha ana simamia na kukamilisha ujenzi wa matundu ya vyoo kwa ushirikishaji wa wananchi wa eneo lake.

Kwa upande wake Mkuu wa maendeleo ya jamii Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga ,John Tesha amesema Serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja na yapo yanayowezekana kwa nguvu ya wananchi na serikali.

"Utamaduni wa kujitolea upo katika maisha yetu kwa maendeleo mbalimbali hasa harusi,ila changamoto ya jamii inakuja unapo waambia kuchangia vyoo,madarasa nk.,Hivyo basi ni wakati wa kubadili mitizamo kwa jamii zetu" Alisema Tesha.

Akihitimisha kikao hicho cha uzinduzi wa mradi wa Hisani kwa jamii,Tedson Ngwale,Afisa Maendelo mkoa wa Shinyanga amesema rasilimali zote ziko ndani ya jamii na suala la ushirikishwaji linahitajika.

" Mimi ni mfuasi na muuni wa ushirikishaji wa wananchi katika maendeleo yao,Serikali ya mkoa imepokea mradi huu na tuko tayari kutoa ushirikiano pale mtakapo tuhitaji" Amesema Ngwale.

Mgeni rasmi Chila Moses ambaye ni afisa Mipango na uratibu kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, aliyemwakilisha katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary wakati wa uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( Community Philanthropy)

Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa Hisani katika jamii( community Philanthropy).

Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Afrika Initiatives (TAI) Jonathan Manyama akitoa maelekezo juu ya mradi huo.

Mkurugenzi wa shirika la Thubutu Afrika Initiatives (TAI) Jonathan Manyama akitoa maelekezo juu ya mradi huo.
Afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga John Tesha akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Afisa Mradi kutoka shirika la Thubutu Afrika Initiatives (TAI). Paschalia Mbuguni akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia mradi wa Hisani katika jamii Joseph Ndatala akizungumza baada ya kuchaguliwa
 
 Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala akichangia hoja juu ya mradi huo.

Diwani wa kata ya Lubaga Reuben Dotto akichangia hoja kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Wajumbe wa kamati ya kusimamia kamati ya kusimamia mradi wa Hisani katika jamii wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Post a Comment

0 Comments