Header Ads Widget

SHINYANGA WAFANYA KIKAO CHA TATHIMINI UTEKELEZAJI MPANGO WA TAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO, MILA, DESTURI BADO KIKWAZO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha Tathimini cha MTAKUWWA.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga imefanya kikao cha kutathimini utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA), huku ikielezwa mila na desturi kandamizi bado tatizo mapambano vitendo hivyo vya ukatili.

Mpango mkakati huo wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto Tanzania (MTAKUWWA) ulianza mwaka (2017/18-2021/22), lakini Mkoa wa Shinyanga ulianzisha mpango wake mkakati wa miaka mitano, kuanzia (2020-2025) ili kuhakikisha vitendo vyote vya ukatili vinakwisha hasa mimba na ndoa za utotoni.

Kikao hicho kimefanyika leo, Mei13, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kukutanisha waratibu wa MTAKUWWA kwa kila Halmashauri, na wadau ambao wanahusika moja kwa moja kwenye utekelezaji wa mpango huo wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, amesema kutokana na jitihada za wadau kuendelea kupambana kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kushirikiana na Serikali, imesababisha mkoa huo kushuka kutoka nafasi ya kwanza katika matukio ya ukatili hadi nafasi ya tano kitaifa.

Amesema kwa mujibu wa utafiti wa maendeleo ya watu na afya (TDHS) (2010) ilionekana Mkoa huo wa Shinyanga kuongoza kitaifa kwa tatizo la ndoa za utotoni asilimia 59 na mimba za utotoni asilimia 34.

Aidha, alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), kuwa kwa utafiti ambao waliufanya mwaka (2020-21) Mkoa huo umeshuka katika matukio yote ya ukatili kutoka kushika nafasi ya kwanza kitaifa hadi ya tano.

“Matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Mkoa huu wa Shinyanga kiasi kikubwa yanasababishwa na mila, desturi kandamizi, uelewa mdogo wa haki za binadamu, na kutotambua athari za ukatili,”amesema Omary.

“Wote mliohudhuria kikao hiki ni wadau muhimu katika mapambano dhidi ya kupinga ukatili wa wanawake na watoto, natoa wito kwenu muendelee kuelimisha jamii juu ya madhara ya mila na desturi kandamizi, na kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wazazi,

“Naamini jamii ikielimika na kuheshimu haki na utu wa kila binadamu, itasaidia kumaliza kabisa matukio ya ukatili na hatimaye kuwa na jamii salama,”ameongeza.


Katika hatua nyingine, ameyapongeza Mashirikia yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo, kwa kazi kubwa ambayo wameifanya ya mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto, kuwa kwa kiasi kikubwa wamesaidia katika mapambano hayo ya kupinga ukatili mkoani humo.

Kwa upande wa wajumbe waliohudhuria kikao hicho, kwa nyakati tofauti wakizungumza kwenye majadiliano, wamesema matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuendelea mkoani humo, yanatokana na sababu mbalimbali ikiwamo mila na desturi pamoja na jamii kutotoa ushahidi Mahakamani ili wahusika wapewe adhabu na kuwa fundisho kwa wengine.

Naye Mratibu wa mpango huo wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, ametaja dira ya taifa ya kutokomeza ukatili huo kuwa ni jumuishi ikiwamo Magereza, Polisi, Mahakama na wadau wengine wa kupinga vitendo vya ukatili.

Ametaja pia maeneo nane ya mkakati huo katika kupambana na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kuwa ni kuimarisha uchumi wa Kaya, kupinga mila na desturi kandamizi, mazingira salama sehemu za umma, malezi makuzi na mahusiano ya familia, utekelezaji na usimamizi wa sheria, utoaji huduma kwa wahanga wa ukatili.

Mazingira salama shuleni na stadi za maisha, pamoja na uratibu ufuatiliaji na tathimini.

Katika kikao hicho kimehudhuliwa na Ofisi ya Mashitaka ya Serikali mkoa wa Shinyanga, Mahakimu, Mawakili, Jeshi la Polisi, Waratibu wa Mtakuwwa, Wakurugenzi wa Halmashauri wadau kutoka Shirika la Msaada wa kisheria PACESH, Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) na Mwenyekiti wa Baraza la watoto Taifa Nancy Kasembo, na kikao hicho kimefadhiliwa na Shirika la mpango wa maendeleo Duniani UNFPA.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya.

Wakili wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Mashitaka mkoani Shinyanga Wampumbulya Shani, akiwasilisha taarifa kwenye kikao hicho.

Mratibu wa MTAKUWWA mkoani Shinyanga Tedson Ngwale akiwasilisha taarifa kwenye kikao hicho..

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando akizungumza kwenye kikao hicho.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga Mary Mrio akizungumza kwenye kikao hicho.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Shinyanga Ushindi Swalo akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwandishi wa Habari AZAM TV mkoani Shinyanga Kasisi Kosta akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa Baraza la watoto Taifa Nancy Kasembo akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary (kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Tomothy Ndanya kwenye kikao hicho cha Tathimini cha MTAKUWWA.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akiwa kwenye kikao hicho.

Wajumbe wakiendelea na kikao.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments