Header Ads Widget

SHEIKH MAKUSANYA AONGOZA SWALA YA EID EL-FITRI, RC MJEMA AWASIHI WATANZANIA KUMUOMBEA RAIS SAMIA, KUJITOKEZA KUHESABIWA SENSA

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akiongoza swala ya Eid El- Fitri.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHEIKH wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya, ameongoza waumini wa dini ya Kiislamu mkoani humo katika Swala ya Eid El-Fitri, huku akiwataka Waumini wa dini hiyo pamoja na watazania wote kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Swala hiyo ya Eid El-Fitri mkoani Shinyanga imefanyika leo Mei 3, 2022 katika viwanja vya michezo vya Sabasaba Mjini Shinyanga.

Amesema waumini wa dini hiyo na watanzania wote kwa ujumla, wanapaswa kuendelea kudumisha amani ya nchi, kuwa na upendo, utulivu, kushikamana, pamoja na kumuombea Rais Samia aendelee kuwa na afya njema na kuliongoza Taifa vizuri.

“Waumini wa dini ya kiislamu na watanzania wote tunawaomba muundelee kudumisha amani ya nchi, tushikamane, na kumuombea afya njema Rais wetu Samia, pamoja na safari zake zote ziwe za heri na mibaraka sababu anazifanya kwa maslahi ya nchi,”amesema Sheikh Makusanya.

“Waislamu tunapo sherehekea pia Sikukuu hii ya Eid, tuwakumbuke yatima, wajane, wafungwa, na watu wenye ualibino, kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili tupate thawabu kutoka kwa mwenyezi mungu,”ameongeza.

Naye Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategile, aliwasisitiza pia waumini wa dini hiyo ya kiislamu wapendane, kusaidiana na kuhurumiana, na siyo kuishi kama watu wasio mjua Mungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza mara baada ya swala kumalizika amewataka pia Watanzania kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita, kwa shughuli za kimaendeleo ambazo inazifanya, na kumuombea Rais Samia afya njema ili aendelee kuchapa kazi.

“Naomba wananchi wote tuiunge mkono Serikali ya awamu ya sita kwa shughuli zake ambazo inazifanya za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwamo sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, na kilimo, mfano hapa Shinyanga tunatarajia kuwa na mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji na tuna mshukuru sana Rais Samia,”amesema Mjema.

Katika hatua nyingine Mjema, aliwataka wananchi wa mkoa huo wa Shinyanga, siku ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Agost 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa, ili Serikali ipate idadi kamili ya watu wake na kuwa virahisi kutoa huduma kwao hasa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akiongoza swala ya Eid El- Fitri.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akizungumza katika swala ya Eid El- Fitri mkoani humo.

Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategile akizungumza katika Swala ya Eid El-Fitri.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza mara baada ya kumalizika kwa swala ya Eid El-Fitri.

Waumini wa dini ya kiislamu mkoani Shinyanga, wakiwa katika Swala ya Eid El-Fitri.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments