Header Ads Widget

MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE MBELE YA WATOTO NA KUMTOBOA MACHO


Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Ndinyika, Kata ya Karansi wilayani Siha, Stephano Sikawa (33), kwa tuhuma ya kumchinja hadi kumuua mkewe, Sioni Daudi (26), mbele ya mwanawe mwenye umri wa miaka minne.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Simon Maigwa, amesema Sioni aliuawa na mumewe Mnamo Mei 23, 2022 akiwa nyumbani kwake kijijini huko.

"Ni kweli nimepokea taarifa kuhusu mauaji hayo ya kikatili. Mume wa marehemu imebidi tumkamate kwa sababu anahusishwa na mauaji hayo.

Amesema kuwa mtuhumiwa ametekeleza unyama huo kwa kumkata sehemu zake za siri na kuchukua kiungo hicho, akakata viganja vya mkono wa kulia, vidole viwili na kumtoboa macho mwenzi wake huyo.


Imeelezwa kuwa Kuna rekodi ya maneno yake aliyokuwa akiyasema huko nyuma kwamba atamfanya kitu kibaya.


Sasa hivi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa pamoja na Polisi Dawati la Jinsia la Wilaya na OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya) wako wanafuatilia sakata hilo," amesema.
 

Post a Comment

0 Comments