Header Ads Widget

MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA KWENYE KIKAO CHA BARAZA, WAMPATIA CHETI CHA PONGEZI MWANANCHI ALIYETOA ENEO BURE UJENZI WA SHULE

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kushoto) akimpatia Cheti cha Pongezi Mwananchi Mashishanga Kashinje mkazi wa kitongoji cha Mwamagulya Old Shinyanga, kwa kutoa eneo bure kwa ajili ya ujenzi wa shule Shikizi ya Mwamagulya.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Manispaa ya Shinyanga wamewasilisha taarifa za kwenye Kata zao, huku wakibainisha changamoto ambazo bado zinawakabili wananchi na kuhitaji kutatuliwa.

Wamewasilisha taarifa hizo leo Mei 10, 2022 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, ambacho kilikuwa na ajenda ya maswali ya papo kwa papo, kupokea na kujadili taarifa za kwenye Kata.

Madiwani hao kwa nyakati tofauti kila mmoja akiwasilisha taarifa ya kwenye Kata yake, walibainisha changamoto ambazo bado zinawakabili wananchi ikiwamo ubovu wa miundombinu ya barabara, uchakavu majengo ya shule, matundu ya vyoo, kutokamilika ujenzi maboma ya Zahanati, kituo cha Polisi Ngokolo, upungufu wa madawati shule ya msingi Mapinduzi “B” Ngokolo.

Changamoto zingine ambazo zimewasilishwa ni ukosefu Majengo ya Maabara, kujifungua wajawazito hasa katika Zahanati ya Chibe, pamoja na upungufu wa watumishi kwa kila Kata.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani, amesema changamoto zote ambazo zimewasilishwa na Madiwani kwenye taarifa zao zifanyiwe kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amesema tatizo ambalo linakwamisha utatuzi wa changamoto hizo ni upungufu wa Rasilimali fedha, na kubainisha kuwa watakuwa wakizitatua moja baada ya nyingine, na hadi kufikia mwaka 2025 nyingi zitakuwa zimeshatatuliwa.

“Changamoto ambayo inatukabili ni Rasilimali fedha, lakini tutakuwa tukitoa kipaumbele na kutatua tatizo moja baada ya jingine, na hadi kufikia (2025) changamoto nyingi tutakuwa tumezitatua, na zitakuwa za kutafuta na Tochi,”amesema Satura.

Aidha, katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani walimpatia cheti cha Pongezi Mwananchi Saimon Kashinje mkazi wa kitongoji cha Mwamagulya Kata ya Oldshinyanga, kwa kutoa eneo bure Hekari Tano kwa ajili ya ujenzi shule Shikizi ya Mwamagulya.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (katikati) akiongoza kikao cha baraza la madiwani, (kulia) ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, na (kushoto) ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akiongoza kikao cha baraza la madiwani.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Jomaary Satura akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Chibe John Kisandu akiwasilisha taarifa ya kwenye Kata yake.

Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole akiwasilisha taarifa ya kwenye Kata yake.

Diwani wa vitimaalum Pica Chogelo, akiwasilisha taarifa ya Kata ya Ndala kwa niaba ya diwani wa Kata hiyo Zamda Shabani.

Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu akiwasilisha taarifa ya kwenye Kata yake.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya akiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Diwani wa Ibinzamata Ezekiel Sabo akiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha Baraza.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kushoto) akimpatia Cheti cha Pongezi Mwananchi Mashishanga Kashinje mkazi wa kitongoji cha Mwamagulya Old Shinyanga, kwa kutoa eneo bure kwa ajili ya ujenzi wa shule Shikizi ya Mwamagulya.

Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments