Header Ads Widget

KIKUNDI CHA WHATSAPP CHATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO WENYE MTINDIO WA UBONGO KITANGILI SHINYANGA

 
Mratibu wa kikundi cha WhatsApp Together we Fight Gwakisa Mwasyeba (kushoto) akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula katika kituo cha Brothers Of Charity cha kutoa elimu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo kitangili Manispaa ya Shinyanga, (kulia) ni Mkuu wa kituo hicho George Rice.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIKUNDI cha WhatsApp Together we Fight, wametoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula kwa watoto wenye mtindio wa ubongo, ambao wanasoma katika kituo cha Brothers Of Charity kilichopo Kitangili Manispaa ya Shinyanga, huku wakiwataka wazazi kutowaficha watoto wenye ulemavu na kuwapeleka shule.Mratibu wa kikundi hicho cha WhatsApp Gwakisa Mwasyeba, akizungumza leo Mei 14, 2022 wakati wa kutoa msaada huo, amesema wamekuwa na tamaduni ya kusaidia watu wenye uhitaji kila mara, kwa kuchangisha fedha wanakikundi na kutoa misaada mbalimbali ili kuwapa faraja.

Amesema kikundi hicho hua kinatoa misaada kwa wahitaji kila baada ya miezi minne, kwa kuchangishana Sh.10,000 kwa kila mwanakikundi ambao wapo zaidi ya 150, na leo wameamua kutoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula kwa watoto hao wenye matatizo ya utindio wa ubongo.

“Nawashukuru wanakikundi kwa kuendelea kujitoa kuchanga fedha zao na kusaidia watu wenye uhitaji, na hii ni sadaka na kupata Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, sababu watoto hawa wanahitaji faraja kutoka kwetu sisi wanajamii,”amesema Mwasebya.

Aidha, ametaja vitu ambavyo wamevitoa kwa watoto hao wenye matitizo ya utindio wa ubongo kuwa Mchele kilo 200,unga wa mahindi kilo 100, Madaftari box mbili, Juice, pipi, sabuni za unga, mche, biskuti, chumvi, dawa za meno, penseli, pamoja na nguo,

Katika hatua nyingine amekipongeza kituo hicho kwa kusaidia watoto hao wenye utindio wa ubongo na kuwapatia elimu, huku wakitoa wito kwa wazazi ambao wanaishi na watoto wenye ulemavu wasiwafiche ndani, bali wawapatie haki yao ya elimu kama watoto wengine wasio na ulemavu.

Kwa upande wake Mkuu wa kituo hicho cha Brothers Charity, George Rice, amekishukuru kikundi hicho cha Whatsapp kwa kuguswa na watoto hao na kuwapatia msaada huo, na kutoa wito kwa wanavikundi wengine kuiga mfano huo.

Mratibu wa kikundi cha WhatsApp Together we Fight Gwakisa Mwasyeba akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.

Mkuu wa kituo cha Brothers Of Charity George Rice akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo.

Mratibu wa kikundi cha WhatsApp Together we Fight Gwakisa Mwasyeba (kushoto) akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula katika kituo cha Brothers Of Charity cha kutoa elimu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo kitangili Manispaa ya Shinyanga, (kulia) ni Mkuu wa kituo hicho George Rice.

Muonekano wa vitu ambavyo vimetolewa msaada.

Muonekano wa vitu ambavyo vimetolewa msaada.

Misaada ya vitu mbalimbali kikiwamo chakula ikishushwa kituoni hapo.

Misaada ikiendelea kuingizwa ndani ya kituo.

Misaada ikiendelea kuingizwa ndani ya kituo.

Misaada ikiendelea kuingizwa ndani ya kituo.

Misaada ikiingizwa ndani ya kituo.

Misaada ikiingizwa ndani ya kituo.

Mwana kikundi Rose Pesa akikata keki kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kituoni hapo.

Mwanakikundi cha WhatsApp Rose Pesa, akimlisha keki mratibu wa kikundi hicho Gwakisa Mwasyebya katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Mwanakikundi cha WhatsApp Rose Pesa, akimlisha keki Mkuu wa kituo cha Brothers Of Charity George Rice katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo.

Wanakikundi cha WhatsApp Together we Fight wakiwa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo Brothers Of Charity kilichopo Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Wanakikundi cha WhatsApp Together we Fight wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la kutoa msaada katika kituo cha Brothers Of Charity cha watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments