Header Ads Widget

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYANI KAHAMA 'KDFA',KIMEVITAKA VILABU VYA MPIRA KUTIMIZA VIGEZO VYA KUSHIRIKI LIGI YA WILAYA

Katibu wa Chama cha Mpira cha wilaya ya Kahama (KDFA) Fadhil Kipindula (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (katika) ni Tito Okuku Obata na (kulia) ni mwakilishi wa timu za mpira wa wilaya ya Kahama Donarld Igulu

Na Patrick Mabula , KAHAMA.

Chama cha mpira wa miguu cha wilaya ya Kahama , ( KDFA) mkoani Shinyanga kimevitaka vilabu vya mpira kutimiza vigezo vya kushiriki ligi ya wilaya inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi juni mwaka huu kwa kuwa na usajili, katiba , uongozi pamoja na ofisi.

Wito huo umetolewa na katibu wa KDFA , Fadhil Kipindula  alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari katika ofisi ya chama hicho iliyopo uwanja wa Manispaa ya Kahama na kuvitaka vilabu vitakavyo shiriki ligi hiyo kutimiza vigezo na masharti .

Kipindula amesema ligi hiyo inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi juni (6) mwaka huu , jumla ya vilabu 32 ambavyo vinapaswa kuwa vimelipa ada ya uanachama wa KDFA kiasi cha sh.30,000 pamoja na kuwa na Usajili , Uongozi, Katiba na ofisi na kiwanja cha kufanyia mazoezi.

Amesema kwa upande wa gharama za kuendesha ligi hiyo ni kiasi cha shilingi milioni 54 ,zinahitaji huku mdhamini wa michezo hiyo tayari akiwa amepatika ambaye ni Gold Fm na kwa kiasi cha sh.10 milioni .

Kipindula amesema kwa vilabu ambavyo vitakuwa havina katiba amevitaka kuuona uongozi wa wilaya wa KDFA ambao watawasaida kuwadhamini waweze kupata katiba kutoka halmashauri iliko timu hiyo na wasajili wachezaji kwa kufaata taratibu siyo kunyang’anyana wachezaji.

Katibu huyo wa KDFA alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza kudhamini ligi hiyo yenye timu 32 ambapo katika mashindano hayo na timu itakayokuwa mshindi wa kwanza itapata shilingi milioni 5 , wa pili milioni 3 na watatu ataambulia milioni 2.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua wamejipangaje kuhusu malalamiko ya Timu zimekuwa zikiwalalamikia waamuzi , amesema tayari hilo wanalifanyia kazi kuhakikisha halijitokezi kwa kuteua wenye sifa ya kuchezesha ligi hiyo.

Aidha wito wake wa wadau wa michezo wa wilaya ya Kahama , waungane na wawe kitu kimoja kwa kuachana tofauti zao , chuki ,majungu , fitina ambayo yamekuwa yakichelewesha maendeleo ya mpira wilayani hapa.

Post a Comment

0 Comments