Header Ads Widget

MAMA AMZIKA MWANAYE MWENYE ULEMAVU KIMYAKIMYA BAADA YA KUFA NA NJAA

Mama amzika mwanaye kimyakimya usiku baada ya kufa njaa

Mtoto Salah Jackson (5) mwenye ulemavu wa viungo, mkazi wa kijiji cha Makiwaru, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia kutokana na njaa na kisha mama yake mzazi kumzika kimya kimya usiku wa manane.


Mtoto huyo anadaiwa kuzikwa na mama yake mzazi aitwaye Rebecca Siowi (30) usiku wa kuamkia Aprili 22, 2022 nyumbani kwa bibi yake walikokuwa wakiishi yeye pamoja na mama yake baada ya mume kumtelekeza na watoto watano.

Tukio hilo liligundulika baada ya mtoto huyo kutoonekana jioni ya Aprili 21 nyumbani alikokuwa akiishi kwa bibi yake, ambapo bibi yake huyo alifanya jitihada za kumtafuta mjukuu wake huyo bila mafanikio ndipo Aprili 22 alipobainika kuwa amezikwa.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments