Header Ads Widget

ASASI ZA KIRAIA SHINYANGA ZAOMBA WAZIRI GWAJIMA KUWEKA TAKWIMU ZA UKATILI - WEBSITE YA WIZARA

ASASI ZA KIRAI SHINYANGA ZAOMBA WAZIRI GWAJIMA KUWEKA TAKWIMU ZA UKATILI - WEBSITE YA WIZARA.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia,watoto na Makundi Maalum Dkt .Doroth Gwajima akizungumza katika kikao na TAPO la Shinyanga ( umoja wa asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Shinyanga - EVAWC( TAPO),Jonathan Manyama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiative(TAI) akiwasilisha taarifa ya umoja wa asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Jasinta Mboneko alitoa maelezo ya juhudi z serikali katika kutokomeza ukatiki wilaya ya Shinyanga.
Wadau na kutoka serikali na asasi za kiraia walishiriki kikao kazi na waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia,watoto na Makundi Maalum.

 Na Mwandishi wetu.

Umoja wa asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga ( TAPO) umeeleza changamoto zinazokwamisha juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia mkoa wa Shinyanga.

Umoja wa asasi Hizo za kiraia mkoa wa Shinyanga (TAPO)umeleza hayo Leo jumamosi April 23,2022 mbele ya waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi Maalum Dkt.Doroth Gwajima katika kikao kazi kilichofanyika hoteli ya Vigimark manispaa ya Shinyanga.

Waziri Dkt. Gwajima amekutana na umoja wa asasi hizo za kiraia mkoa wa Shinyanga katika ziara yake siku mbili mkoani hapa kutokana na tukio la tarehe 17,Aprili,2022 la mtoto wa kata ya Lyabukande,Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuuliwa na bibi yake .

Waziri Gwajima akiambatana wenyeji wake ambao ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga na Meya wa Manispaa ya Shinyanga katika  kikao cha kukutana na umoja  asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga ( Shy- EVAWC- Working Group)

Mwenyekiti wa umoja wa asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga ,Jonathan Manyama Kifunda ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiative(TAI) aliwasilisha changamoto mbalimbali za asasi hizo juu ya shughuli zao za kupinga kutokomeza ukatili Mkoa wa Shinyanga.

Kifunda alisema changamoto hizo ni pamoja na uchelewaji wa takwimu,ushirikiano mdogo wa baadhi ya watendaji wa Serikali,ukosefu wa rasilimali fedha  katika katika utekelezaji wa MTAKUWWA,ukosefu wa nyumba salama na mabweni ya shule kwa watoto wa kike.

" Mheshimiwa Waziri Dkt.Gwajima,Tunaomba takwimu ziwekwe katika website za wizara Ili kusaidia NGO kupata kutimiza masharti ya haraka ya uombaji wa ruzuku kwa wahisani mbalimbali.Alisema Kifunda.

" Tunakwama kupata taarifa za takwimu za matukio ya ukatili kwa wakati na kukosa fedha za kusaidia mapambano ya ukatili kwa kuwa mchakato wa kupewa taarifa ni mrefu na unachelewa." Alisema Kifunda

Kifunda aliongeza kwa kusema Kuwa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ( MTAKUWWA) unatekelezwa na asasi za kiraia kwa rasilimali fedha kidogo na alishauri serikali kuweka bajeti kwa wizara husika Ili kusaidia Mpango huo kufanikiwa kikamilifu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya SHINYANGA,Jasinta Mboneko alisema kuwa changamoto zote bado serikali inazifanyia kazi Kwa hatua mbalimbali.

" Serikali ya Rais Samia Suluhu imeshatenga fedha kiasi cha Shs bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya bweni kuanzia kidato cha kwanza hadi Cha sita katika eneo la Butengwa manispaa ya Shinyanga ili kusaidia wanafunzi wa kike.

Mboneko pia alizitaka asasi hizo za kiraia kubainisha changamoto zinazo wakwamisha katika utekelezaji wa majukumu yao ambazo zinasababishwa na watendaji wa serikali ili zitafutiwe ufumbuzi,huku akizitaka asasi hizo kutoa elimu kwa watendaji wa serikali ngazi ya kata ili kusaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia,wanawake na makundi maalum Dkt. Doroth Gwajima alisema changamoto zilizowasilishwa na umoja wa asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga (TAPO) ni kweli zipo na kusema zipo zinazo weza kumalizika ngazi ya wilaya na Mkoa na wizara kubaki na zile zenye mfumo wa kisera.

Aidha Dkt.Gwajima alipongeza TAPO la Shinyanga kwa kuwa na umoja huo na pia kuwasilisha taarifa ambayo itasaidia kutoa mwelekeo na kufufua mambo yaliyokuwa hayafanyiki kikamilifu chini ya wizara yake.

"Nitakwenda kuhakikisha tunatoa waraka nchi nzima wa  uwepo na vikao kila robo ya mwaka  kati ya asasi za kiraia na maafisa ustawi na maendelo jamii na pia uwepo wa taarifa za  vikao hivyo kujadiliwa na kuwasilisha kwa wakuu wa wilaya na mikoa Ili kuweza kubaini kipi kinaendelea ndani ya mikoa na wilaya  za juu ya masuala ya ukatili." Alisema Gwajima.

" Pia nitahakisha uwepo wa takwimu katika website ya wizara Ili kusaidia utekelezaji wa majukumu yenu kwa wakati" Alisema Gwajima.

Kwa upande wake Mhe.Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ramadhani Masumbuko alisema kuwa manispaa ya Shinyanga inatoa huduma ya usafiri wa  basi  kwa Sasa Ili kusaidia  wanafunzi wanaotoka mbali kwa gharama nafuu ambayo wazazi na walezi wanaimudu.

Post a Comment

0 Comments