Header Ads Widget

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WALIA UBOVU MIUNDOMBINU YA BARABARA, WAPONGEZA MATUMIZI YA VISHIKWAMBI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wilayani humo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamelalamikia kukithiri kwa ubovu wa miundombinu ya barabara wilayani humo, na kusababishia kukwamisha shughuli za maendeleo.

Madiwani wametoa malalamiko hayo leo April 29, 2022 kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha Robo tatu ya mwaka, wakati wakijadili taarifa wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA.

Walisema barabara nyingi wilayani humo ni mbovu, na zimesababisha shughuli za maendeleo kushindwa kufanyika sababu hazipitiki.

"Ubovu wa miundombinu ya barabara katika halmashauri yetu ya wilaya ya Shinyanga, umekuwa kikwazo kufanyika shughuli za maendeleo," walisema madiwani hao.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, alisema ubovu huo wa barabara zimekuwa pia zikiharibu magari na kuwaingizia gharama za matengenezo pamoja na kutumia mafuta mengi.

Aidha, Mwenyekiti huyo aliagiza Wakala wa Barabara mjini na vijijni (TARURA), kuwaondoa wakandarasi wote ambao ni wazembe wanaotekeleza miradi ya barabara wilayani humo na kuweka wengine wenye uwezo.

"Wakandarasi wote wababaishaji waondoeni, wanakwamisha miradi ya maendeleo, angalieni mikataba yao fuateni taratibu na kuweka wengine ambao wanauwezo," alisema Mboje.

Katika hatua nyingine madiwani hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ngassa Mboje, walipongeza uongozi wa Halmashauri hiyo, kwa kuwapatia madiwani vishikwambi (tablets) ambazo vimekuwa vikiwapatia taarifa za haraka za halmashauri hiyo, pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya karatasi, bali kila kitu kinafanyika kidijitali.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Wakala wa Barabara mjini na vijijini (TARURA) wilayani Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambo, alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha (2021-2022) kuna fedha zimeshatengwa kutengeneza barabara hizo na baadhi wameshapokea na kuanza utekelezaji.

Alifafanua kuwa fedha za ukarabati wa barabara ambazo zimetengwa kwa mwaka huo wa fedha ni Sh.bilioni 1.2 , na wameshapokea Sh. milioni 973,9, fedha za barabara zitokanazo na maendeleo ya jimbo Sh. milioni 500 na wamepokea milioni 450, fedha zitokanazo na tozo ya mafuta ni Sh.bilioni moja na wamepokea milioni 637.

Aidha, katika baraza hilo walijadili taarifa mbalimbali zikiwamo za miundombinu ya barabara, umeme, maji, kilimo na elimu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wilayani humo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Stewart Makali, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Kaimu Meneja Wakala wa Barabara mjini na vijijini (TARURA) wilayani Shinyanga Mhandisi Salvatory Yambo, akisoma taarifa ya TARURA kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, (katikati) akiendesha kikao cha Baraza la Madiwani wilayani humo, (kushoto) ni Makamu Mwenyekiti Issack Sengerema akipitia taarifa mbalimbali kwenye Baraza hilo kwa kutumia kishikwambi, (kulia) ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Stewart Makali.

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, wakipitia taarifa mbalimbali kwa kutumia vishikwambia na siyo kubeba makablasha kama zamani, bali wanaendelea na kikao kwa njia ya digitali.

Diwani wa Masengwa Nicodemas Simoni akipitia taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kwa kutumia kishikwambi.

Diwani wa Itwangi Sonya Mhela akipitia taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kwa kutumia kishikwambi.

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa na vishikwambi kwenye kikao cha Baraza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments