Header Ads Widget

WOMEN FOR CHANGE WATOA MSAADA WA MADAWATI 30 SHULE YA MSINGI LUBAGA, DC MBONEKO AWAPONGEZA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA ELIMU


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akipokea Madawati 30 ambayo yametolewa na kikundi cha wanawake Women For Change, kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Ansila Benedict, kwa nyuma ni wanachama wa kikundi cha Women For Change.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIKUNDI cha Wanawake Women For Change, wametoa msaada wa madawati 30 katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga, huku Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwapongeza pamoja kuwa unga mkono kwa kutoa Kiti na Meza kwa ajili ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wanawake Women For Change Ansila Benedict, amesema kila mwaka wamekuwa wakifanya Sherehe ya wanawake (Women’s Day Out), ambapo kabla ya Sherehe hiyo wamekuwa na utamaduni wa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yakiwamo Madawati shuleni, kupitia mfuko wao wa kuchangia watoto na jamii.

Alisema kupitia mfuko huo, mwaka juzi walikarabati bweni la wanafunzi katika kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga, na mwaka jana walitoa Madawati 50 katika shule ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga, ambapo mwaka huu wametoa madawati 30 katika shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga yenye thamani ya Sh. milioni 2.1.

“Kikundi chetu cha Women For Change, kabla ya kufanya Sherehe yetu ya Women’s day Out, hua tuna utaratibu wa kurudisha fadhila kwa jamii kupitia mfuko wetu wa kuchangia watoto na jamii na kutoa misaada mbalimbali,”alisema Benedict.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekipongeza kikundi hicho cha wanawake Women For Change, kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kutatua changamoto za elimu, huku akiwaunga mkono kwa kutoa zawadi ya kiti na meza kwa ajili ya matumizi ya mwalimu Mkuu wa shule hiyo.

Alisema Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Stella Halimoja amempatia zawadi hiyo kutokana kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya darasa la Saba kwa shule za Serikali Manispaa ya Shinyanga.

Alisema shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa madawati 73, ambapo 30 yamepatikana na kusalia 43, ambayo yatamaliziwa na Serikali na tayari yapo katika chuo cha ufundi Veta yakitengenezwa.

Aidha, alisema mkakati wa Serikali kwa Shule zote za Manispaa ya Shinyanga na halmashauri ya wilayani Shinyanga, ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi ambaye atasoma akiwa hawa dawati, kiti wala meza, ambapo zoezi hilo kwa shule za Sekondari wamemaliza na sasa wanaelekeza nguvu kwa shule Msingi.

Pia amewapongeza walimu wa shule hiyo ya Lubaga kwa kujituma kufundisha wanafunzi, na kushika nafasi ya kwanza kwenye Matokeo ya darasa la Saba kwa shule za Serikali Manispaa ya Shinya, na kuwasihi waendelee na kasi hiyo hiyo, huku akiwataka na wanafunzi wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao na kuja kuwa viongozi wa taifa hili hapo baadae.

Alisema kwa changamoto ambayo bado inaikabili shule hiyo ikiwamo upungufu wa viti na meza kwa walimu, ameahidi kuwa atalitatua huku akiwataka na walimu katika shule nyingine za Serikali wajitahidi kufundisha wanafunzi na watakaofanya vizuri watapewa zawadi.

Katika hatua nyingine Mboneko amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kutoa fedha kiasi cha Sh. milioni 600 kwa ajili ya kujenga Shule mpya ya Sekondari Lubaga, na wameshapokea fedha Sh. milioni 470 na ujenzi unaendelea, shule ambayo itawaondolea changamoto wanafunzi ya kusoma umbali mrefu.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Stella Halimoja, amekishukuru kikundi hicho cha Women For Change, kwa kuwapatia msaada huo wa Madawati 30 ambayo yatapunguza upungufu uliopo wa madawati shuleni hapo, pamoja na mkuu huyo wa wilaya kwa kumpatia zawadi ya kiti na meza.

kikundi hicho cha Women For Change kimeungwa mkono na wadau mbalimbali katika kufanikisha sherehe yao ya Women’s day Out ambayo itafanyika jumamosi, wakiwamo Winterfell, Little Treasures School, Hilbat Pre and primary School, Msilikare Micro Credit, Shybest, Beirbamas Travel Agent, Jambo, Mama Diariesm VRK Traders, Diamon Royal Hotel, UTT Amis, Bwihas, Fk Grand kitchen,Lulekia Company, BM Investment, Jeminaely home Shoping Center.

Wengine ni Mama Kweka House of Tiles, Hahosa Stationary, St Joseph Collenge, Sheer Bills School, Vai Saloon, Mama Love Decoration, Ommy Fashion, Bonga Security, Ekisha Printing, Brother hood, Kom School, Shuwasa, Lope Catering, Dewin Cake pamoja na Hope Extended Secondary Secondary.

Kauli mbiu yao ya mwaka huu kwenye sherehe hiyo ya wanawake inasema WOMEN’S DAY OUT, “Amka, Futa chozi, Pambana, 2022 twende pamoja”.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya madawati 30 katika Shule ya msingi Lubaga kutoka katika kikundi cha wanawake Women For Change.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake Women For Change Ansila Benedict, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi madawati 30 katika Shule ya msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Sherehe ya wanawake Women's day Out, Faustina Kifambe, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi madawati 30 katika shule ya Msingi Lubaga

Afisa Elimu Shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kupokea Madawati 30 katika Shule ya msingi Lubaga kutoka kwenye kikundi cha wanawake Women For Change, pamoja na Kiti na Meza kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Diwani wa Lubaga Luben Dotto, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kupokea Madawati 30 katika Shule ya msingi Lubaga kutoka kwenye kikundi cha wanawake Women For Change, pamoja na Kiti na Meza kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga Stella Halimoja, akitoa shukrani kwa kupata Madawati hayo 30 kutoka kwenye kikundi cha Wanawake Women For Change, pamoja Kiti na Meza kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akipokea Madawati 30 ambayo yametolewa na kikundi cha wanawake Women For Change, kushoto ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Ansila Benedict, kwa nyuma ni wanachama wa kikundi cha Women For Change.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akimkabidhi Madawati 30 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga Stella Halimoja, ambayo yametolewa na kikundi cha wanawake Women For Change.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akimkabidhi Kiti na Meza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga Stella Halimoja.

Wanafunzi wakiwa wamekalia Madawati.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa pamoja na wanakikundi cha Women For Change wakiwa wamekalia Madawati.

Muonekano wa Madawati 30 ambayo yametolewa na kikundi cha Women For Change katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa Madawati ambayo yametolewa na kikundi cha Women For Change katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Awali kikundi cha Wanawake Women For Change, wakiwa kwenye Hafla fupi ya kukabidhi Madawati 30 katia Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Ansila Benedict, (wa kwanza pichani aliyekaa kwenye kiti).

Picha ya pamoja ikipigwa na wanafunzi mara baada ya kumaliza makabidhiano ya Madawati 30 katika Shule ya Msingi Lubaga yaliyotolewa na Women For Change, pamoja Kiti na Meza vilivyotolewa kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Picha ya pamoja ikipigwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lubaga Stella Halimoja mara baada ya kumaliza makabidhiano ya Madawati 30 katika Shule hiyo, pamoja na Kiti na Meza.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifurahi pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Lubaga kwenye Hafla fupi ya makabidhiano ya Madawati 30 shuleni hapo, pamoja na Kiti na Meza.

Wanakikundi cha Women For Change wakifurahi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Lubaga kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi Madawati 30.

Wanakikundi cha Women For Change wakifurahi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Lubaga kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi Madawati 30.

Wanakikundi cha Women For Change, wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,  (mwenye kofia katikati) mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo fupi ya kukabidhi Madawati, Kiti na Meza katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Wanakikundi cha Women For Change, wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,  (mwenye kofia katikati) mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo fupi ya kukabidhi Madawati, Kiti na Meza katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Wanakikundi cha Women For Change, wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (mwenye kofia katikati) mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo fupi ya kukabidhi Madawati, Kiti na Meza katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Wanakikundi cha Women For Change, wakipiga picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (mwenye kofia katikati) mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo fupi ya kukabidhi Madawati, Kiti na Meza katika Shule ya Msingi Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Awali wanakikundi cha Women For Change, wakiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wakiwasili kwenye Shule hiyo ya Msingi Lubaga kwa ajili ya kukabidhi Madawati 30, pamoja Kiti na Meza.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments