Header Ads Widget

WACHIMBAJI WADOGO KAHAMA WAPATIWA ELIMU YA USIMAMIZI NA USALAMA MIGODINI.

WACHIMBAJI WADOGO KAHAMA WAPATIWA ELIMU YA USIMAMIZI NA USALAMA MIGODINI.


 Picha ya pamoja ya viongozi wa wachimbaji wadogo na maafisa kutoka tume ya madini nchini wakati wa mafunzo ya usimamizi na usalama migodini yaliyofanyika wilaya ya kahama leo hii.

  Winnifrida Mrema meneja  ukaguzi wa migodi  kutoka tume ya madini nchini akichukua taarifa wakati wa kikao.

        

Wachimbaji wa madini kutoka wilaya ya Kahama walioshiriki mafunzo ya usimamizi na usalama migodini kutoka  tume ya madini Tanzania.
Kamanda wa jeshi la zimamoto  wilaya ya Kahama  Inspector Hanafi Nkilindi akielezea namna ya zoezi la usalama na uokoaji mgodini.

Kaimu  mkurugenzi ukaguzi migodini na Mazingira  Henry Mditi  akiongea na wachimbaji wadogo  kuhusu Sheria na kanuni za usalama ,usimamizi wa mgodi,uteuzi na mamlaka ya meneja mgodini.


Joseph Nalimi -Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo  wilaya ya Kahama akizungumza juu wakati wa mafunzo ya usimamizi na usalama kwa  wachimbaji wadogo.

Katibu Tawala wilaya ya Kahama,Timothy Ndanya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.

Na Neema Sawaka,


WACHIMBAJI wadogo  na viongozi wanaosimamia  migodi  kwa mkoa wa kimadini Kahama wamepatiwa elimu juu ya  usimamizi  wa mgodi ,Sheria na kanuni za usalama ,uteuzi na mamlaka ya meneja  mgodini .

Mafunzo hayo yametolewa leo machi 11,2022 na wataalamu kutoka tume ya madini  nchini ambapo mgeni rasmi akiwa katibu tawala wilaya ya  Kahama Timothy Ndanya  kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga .

Dkt Anorld Gesesa  mkurugenzi wa huduma za sheria kutoka tume ya madini amesema kuwa  Sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa  marekebisho yake  mwaka 2017  na kanuni  zake nyingi ambazo  wachimbaji wadogo wamekuwa hawazifuati na kuwasababishia madhara endapo wakizifuata wangeweza kuepuka madhara yote yanayotokea kwa watu.

Winnifrida Mrema ambaye ni meneja ukaguzi wa  migodi  kutoka tume ya madini amesema kuwa wachimbaji wamekuwa wakifanya kazi za mazoea  bila kuzingatia sheria za usalama mahali pa kazi  ambapo shughuli za mgodini maeneo siyo salama hivyo yameweza kusababisha vifo .

"Hatutaki maeneo ya uchimbaji yasiwe salama   tunataka yawe salama na wachimbaji wafanye kazi kwenye maeneo salama na wanaosimamia wanatakiwa wazingatie Sheria ili kuweza kuwavusha salama na mkakati wa kusanifu mgodi  watumike wataalamu waziri ili kubuni muundo na usanifu  katika eneo husika" amesema Mrema.

Mhandisi Henry  Mditi Kaimu mkurugenzi ukaguzi  migodini  na mazingira  kutoka tume ya madini amesema kuwa  uteuzi na mamlaka ya mameneja mgodini  ni upo kisheria  na mgodi haupaswi kufanya kazi zaidi ya siku saba bila kuwa na meneja mgodi.

"Sheria  ya madini sura ya 123 na kanuni za uchimbaji  mdogo  za mwaka 2010 zimeainisha mambo ya msingi ya kuzingatia katika usimamizi wa afya,usalama na utunzaji wa mazingira kabla ya kuanza  uchimbaji,wakati wa uchimbaji na baada ya uchimbaji."amesema mhandisi Mditi.

Ofisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini Kahama Jeremiah Hango amesema kuwa  mkoa una jumla ya  leseni za uchimbaji   mdogo 592 ambapo  leseni za utafutaji  madini zipo leseni 65 Kati ya hizo zipo baadhi  katika hatua ya awali.

Mgeni rasmi katibu tawala wilaya ya Kahama  Timothy Ndanya amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa wachimbaji hawa ni  kuripotiwa wizi wa carbon ambapo mtu akibainika uongozi wa wilaya hautamvumilia kumfutia leseni na wengi wao wamekuwa hawafuati sheria na taratibu zilizopo.


Post a Comment

0 Comments