Header Ads Widget

RC MJEMA AKOSHWA KIKUNDI CHA WANAWAKE WENYE ULEMAVU KUCHANGAMKIA MIKOPO YA HALMASHAURI NA KUJIKWAMUA KIUCHUMI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akiwa kwenye Banda la Wajasiriamali la wanawake wenye ulemavu wilayani Kahama, akisikiliza maelezo namna walivyo nufaika na mkopo wa Halmashauri asilimia Mbili kuwa kwamua kiuchumi, (kushoto) ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Rehema Mkengele.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amekipongeza kikundi cha wanawake wenye ulemavu wilayani Kahama, kwa kuchangamkia mikopo ya Halmashauri asilimia mbili za watu wenye ulemavu, na kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi.

Mjema, ametoa pongezi hizo leo, alipokuwa akikagua mabanda ya wanawake wajasiriamali, mashirika mbalimbali na Taasisi za kifedha, kwenye maonesho ya wajasiriamali wilayani Kahama, katika wiki ya maadhimisho ya wanawake duniani ambapo kilele chake ni kesho.

Alisema amefurahishwa na kikundi hicho cha wanawake wenye ulemavu, kwa kujituma kufanya kazi na kujipatia kipato na kuachana na dhana ya kuwa tegemezi, huku akitoa wito kwa watu wengine wenye ulemavu wachangamkie fursa za mikopo za Halmashauri na kujikwamua kiuchumi.

“Kikundi hiki nataka sasa mkawe mabalozi kwa wenzenu wenye ulemavu, kuwa mikopo ipo ya Halmashauri asilimia mbili kwa ajili yao, na siyo lazima kujiunga kwenye kikundi cha watu wengi, bali ni wachache tu kama mlivyo ninyi watatu, ambapo kwa sasa mnafanya shughuli zenu na kupata kipato,”alisema Mjema.

Pia, alitoa wito kwa wanawake mkoani humo wajiunge kwa wingi kwenye vikundi vya ujasiriamali, ili wapate mikopo ya Halmashauri asilimia 4 na kupata mitaji ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kuliko kukaa bila ya kufanya kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi hicho cha wanawake wenye ulemavu Rehema Mkengele, alisema kikundi chao kinaitwa Amani, na walipata mkopo wa halmashauri Sh.milioni 10 mwaka jana, na kuanza shughuli za ununuaji mazao ya Mpunga, Mahindi,Kalanga na Alzeti.

Alisema baada ya kununua mazao hayo na kuuyauza, pia wamekuwa wakitumia malighafi ya mazao hayo kutengenezea bidhaa mbali mmbali yakiwamo mafuta ya kula ya Alzeti, Peanut Butter za kulia mikate zitokanazo na Kalanga, na wamekuwa wakifanya shughuli nyingine za kufuma mashuka na kuuza.

Naye Katibu wa kikundi hicho Letisia Kapwani, aliipongeza Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa fedha hizo za mikopo ya wajasiriamali kupitia Halmashauri, ambayo imekuwa msaada mkubwa sana kwao katika kujikwamua kiuchumi, na kubadili mfumo wa maisha yao na kuacha kuwategemezi tena.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akiwa kwenye Banda la Wajasiriamali la wanawake wenye ulemavu wilayani Kahama, akisikiliza maelezo na kuangalia bidhaa zao ambazo wanazitengeneza na kuwa kwamua kiuchumi, (kushoto) ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Rehema Mkengele.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga, wakiangalia bidhaa mbalimbali kwenye kikundi cha wanawake wenye ulemavu kwenye maonesho ya ujasiriamali wilayani Kahama.
 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiangalia bidhaa za wanawake wajasiriamali kwenye maonesho ya wajasiriamali wilayani Kahama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA.

Post a Comment

0 Comments