Header Ads Widget

STEPHEN WASIRA AFUNGUKA URAIS 2025

Mwanasiasa mkongwe nchini, Stephen Wasira, amesema Rais Samia aachwe amalizie vipindi viwili vya urais kama ilivyo utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Aliyasema hayo jana mkoani Mara alipopewa nafasi ya kuzungumza baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa chujio la maji wilayani Bunda.

“Wale waliosema wanataka urais 2025, mimi nawashauri wasubiri kwa sababu kwa utamaduni wa CCM kama kuna rais aliyepo ofisini huwa hatumpingi, tunampa nafasi amalizie awamu hiyo ambayo ni miaka 10,” alisema Wasira.

Alitoa mfano wake binafsi kwamba aliwania urais, lakini hakuupata na sasa kwa kuwa ameshapitwa na umri, amekaa pembeni na hana nia tena ya kuwania.

Wasira aliwataka wenye dhamira hiyo ya urais wasubiri hadi vipindi viwili vya Rais Samia vipite, na iwapo watakuwa wamepitwa na umri waige mfano wake, ambaye amejiunga na wazee wa Mara maana si wote lazima kuwa rais bali ni fursa ya mtu mmoja.

                     SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MPEKUZI.

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807