Header Ads Widget

SHIRIKA LA AGAPE, HER DIGNITY WAENDESHA MIKUTANO YA URAGBISHI KUIBUA MASUALA YANAYOSABABISHA UKATILI KWENYE VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MGODI WA MWADUI

Mratibu wa Miradi kutoka Shirika la AGAPE Peter Amani, akizungumza kwenye mkutano wa Ulagbish katika kijiji cha Buchambi wilayani Kishapu, wa kuibua changamoto za wananchi ambao wanaishi kwenye vijiji vinavyozungukwa na Mgodi wa Mwadui na kusababisha matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

SHIRIKA LA AGAPE na HER DIGNITY, wameendesha mikutano ya hadhara ya Ulagbishi katika vijiji vya Buchambi na Buganika wilayani Kishapu, ambavyo vinazungukwa na Mgodi wa madini ya Almasi Mwadui, ili kuibua changamoto ambazo hua zinawakabili na kusababisha kuibuka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mikutano hiyo imefanyika leo February 24, 2022 kwa nyakati tofauti, kwa kushirikisha wananchi wenyewe kuibua changamoto zao, na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.

Mratibu wa miradi kutoka Shirika hilo la AGAPE Peter Amani, alisema mradi huo wanautekeleza ndani ya miezi 11, ambapo watazunguka vijiji vyote 11 ambavyo vinazungukwa na Mgodi huo wa Madini ya Almasi Mwadui, kwa kuibua changamoto ambazo zinawakabili wananchi na kutafutwa ufumbuzi, ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ambayo yanatokana na changamoto hizo.

“Mradi huu wa Ulagbishi tunautekeleza Shirika la AGAPE kwa kushirikiana na Shirika la HER DIGNITY, kwa kuibua changamoto ambazo jamii inayozunguka Mgodi huu wa Mwadui zinawakabili, na kusababisha kutokea vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,”alisema Amani.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza, alisema utekelezaji wa mradi huo watakuwa wakishirikiana na wananchi wenyewe kuibua changamoto zao, pamoja na kuunda kamati za wajumbe wawili kwa kila kijiji ambao watakuwa wakishirikiana na Walaghbishi wawili wa kila kijiji ambao wamepewa mafunzo namna ya kushughulika na matatizo ndani ya jamii.

Nao Wananchi wa vijiji hivyo viwili vinavyo zungukwa na Mgodi wa Mwadui, kwa nyakati tofauti walibainisha changamoto ambazo zinawakabili na kusababisha matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, kuwa ni ukosefu wa maji safi na salama na umbali wa shule.

Changamoto zingine zilizoibuliwa, ni ukosefu wa huduma bora za Afya na kusababisha baadhi ya Wajawazito kupata Shida wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Mahusiano ndani ya Mgodi huo wa Madini ya Almasi Mwadui Hilda Hizza, Alisema kwa upande wa utekelezaji wa shughuli mbalimbali ndani ya jamii inayozunguka mgodi huo, hua kuna fedha za mzunguko ambazo hutolewa kila mwaka, ambapo wananchi wenyewe ndiyo wanapaswa kukaa kwenye mkutano wa hadhara, na kutoa kipaumbele chao nini wanahitaji kutekelezewa na Mgodi, na wao huwatekelezea kulingana na mahitaji yao.

Alifafanua kuwa baadhi ya vijiji waliomba miradi ya maji na wameshatekelezewa na wengine waliomba Ofisi ya kijiji wakafanya hivyo pia, na kutoa ushauri kwa wananchi wanapokuwa wakikaa kwenye mikutano hiyo wainishe kipaumbele ambacho ni muhimu ili watekelezewe ikiwamo miradi hiyo ya maji safi na salama.

Mratibu wa Miradi kutoka Shirika la AGAPE Peter Amani, akizungumza kwenye mkutano wa Ulagbish katika kijiji cha Buchambi wilayani Kishapu.
Mkurugenzi wa Shirika la HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza, akizungumza kwenye mkutano huo wa Ulaghbishi wa kuibua changamoto za wananchi katika kijiji cha Buchambi, ambao wanaishi kwenye vijiji vinavyozungukwa na Mgodi wa Mwadui na kusababisha matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la HER DIGNITY Annagrace Rwehumbiza, akizungumza kwenye mkutano huo wa Ulaghbishi wa kuibua changamoto za wananchi katika kijiji cha Buganika ambao wanaishi kwenye vijiji vinavyozungukwa na Mgodi wa Mwadui na kusababisha matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Wananachi wa kijiji cha Buchambi wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa Ulaghbishi, wakuibua changamoto ambazo zinawakabili na kusababisha matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Wananachi wa kijiji cha Buganika wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa Ulaghbishi, wakuibua changamoto ambazo zinawakabili na kusababisha matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mwananchi wa kijiji cha Buchambi Agnes Charles, akielezea changamoto ambazo zinawakabili kwenye kijiji hicho na kusababisha matukio ya ukatili kuwepo.
Mwananchi wa kijiji cha Buganika Rebeka Elias, akielezea changamoto ambazo zinawakabili kijijini humo na kusababisha matukio ya ukatili.

Wananchi wakiendelea kuelezea changamoto ambazo zinawakabili kwenye vijiji vyao na kusababisha matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Na Marco Maduhu, KISHAPU.

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807