Header Ads Widget

MBUNGE KIGWANGALLA AMPINGA WAZIRI BASHUNGWA UJENZI MAKAO MAKUU HALMASHAURI YA WILAYA YA NZEGA




Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamisi Kigwangalla

Wakati Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa akielekeza Makao Makuu ya halmashauri ya Wilaya ya Nzega yajengwe Lubisu badala ya Ndalla, Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamisi Kigwangalla, amesema atakwenda mahakamani kupinga agizo hilo.

Wiki iliyopita Waziri Innocent Bashungwa aliwaita viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Nzega Vijijini Jijini Dodoma na kuwaeleza eneo linalotakiwa kujengwa makao makuu ya halmashauri.

Miongoni mwa viongozi waliofika katika kikao cha Waziri Bashungwa ni pamoja na Dk Kigwangala, Mwenyekiti wa Halmashauri Henerico Kanoga na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba.

Akizungumza na wakazi wa Tarafa ya Puge katika kata ya Ndalla jana Februari 21, Kingwangalla amesema mchakato, sheria na kanuni hazijafuatwa na wala nguvu ya hoja haijaangaliwa katika kuamua sehemu ya kujengwa Makao Makuu ya halmashauri.

SOMA ZAIDI HAPA ;CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments