Header Ads Widget

GAMING BODI YATEKETEZA MASHINE ZA MILIONI 70 MICHEZO YA KUBAHATISHA UKWEPAJI KULIPA MAPATO YA SERIKALI


Mashine za michezo ya kubahatisha zikiteketezwa Moto

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BODI ya michezo ya kubahatisha Tanzania (Gaming Board), imeteketeza mashine 33 ya michezo hiyo, kutokana na kukeuka sheria na ukwepaji wa kulipa mapato ya Serikali.

Mashine hizo za michezo ya kubahatisha zilikamatwa katika oparation iliyoendeshwa na bodi hiyo katika Manispaa ya Shinyanga Januari mwaka huu, ambazo zina thamani ya Sh. Milioni 70.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania James Mbalwe, akizungumza leo na waandishi wa habari, alisema wamekamata mashine hizo kutokana na kukeuka taratibu za uendeshaji wa michezo hiyo.

Alisema mashine hizo 33 ambazo wamezikamata ndani ya mwezi huo mmoja katika Manispaa ya Shinyanga, zimeikosesha Serikali mapato ya Sh. milioni 3.6.

"Baada ya kuzikamata mashine hizi wamiliki wake walikimbia na kuzitelekeza na tulipozifungua ndani tumekuta zina kiasi cha fedha Sh.milioni 1.6 ambazo tunazitaifisha," alisema Mbalwe.

Aidha, alisema kwa mujibu wa Sheria mara baada ya kuzikamata mashine hizo, wanapaswa kuzitekeza moto na ndicho ambacho wamekifanya, ili kutoa fundisho kwa watu wengine, ambao wanaendesha michezo hiyo kinyume cha sheria na ukwepaji kodi za Serikali.

Katika hatua nyingine, alitoa onyo kwa wale ambao wanaendesha michezo hiyo ya kubahatisha, kuwa ni marufuku kuruhusu watoto kuicheza, wala kuiweka karibu na maeneo ya Shule na Hospitali.


Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania James Mbalwe,akiwa kwenye eneo la kuteketeza mashine za michezo hiyo ya kubahatisha.

Mashine zikiteketezwa Moto.

Awali Mashine za michezo ya kubahatisha zikishushwa kwa ajili ya kuteketezwa Moto.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments