Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAPEWA MAFUNZO YA UFEMINIST KUTOKOMEZA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Afrika Intiatives mkoani Shinyanga, akitoa mafunzo ya ufeminist kwa waandishi wa habari 15 ambao wapo kwenye timu ya kuandika habari za kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAANDISHI wa habari 15 mkoani Shinyanga, ambao wapo kwenye Timu ya kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamepewa mafunzo namna ya kuandika habari za (ufeminist) katika kumkomboa mwanamke na mtoto dhidi ya matukio ya ukatili kupitia kalamu zao.

Mafunzo hayo yameendeshwa leo Januari 22, 2022 ikiwa ni maandalizi ya kwenda kutekeleza mradi wa nafasi ya vyombo vya habari katika kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mradi ambao utatekelezwa na waandishi wa habari kwa muda wa miezi mitatu katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kwa ufadhili wa mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT) wenye thamani ya Sh.milioni 16.7

Akitoa mafunzo hayo ya ufeminist mwezeshaji Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Afrika Intiatives , alisema dhana ya ufeminist ni harakati za ukombozi wa mwanamke kimapinduzi, katika masuala ya siasa, uchumi, kitamaduni na ustawi wa jamii ,ambapo wanaandishi habari wanauwezo mkubwa wa kutumia kalamu zao kumkomboa mwananake na mtoto.

“Waandishi wa habari mnanguvu sana katika kumkomboa mwananke na mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kupitia kalamu zenu, hivyo naombeni muishi sana kwenye dhana ya ufeminist wakati wa utekelezaji wa majukumu yenu,”alisema Mbugani.

Kwa upande wake Mwandishi wa Habari Mwandamizi Kareny Masasy, akitoa mada kuhusu kalamu ya uandishi wa habari na ufeminist, amewataka waandishi wa habari, wanapokuwa wakiandika habari zao za kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, wazingatie takwimu , sera na bajeti ili kuzipa uzito habari zao.

Masasy alisema kuwa waandishi wote wa habari ni wafeminist, sababu wamekuwa wakiandika habari za kuibua na kuripoti matukio mbalimbali, na baadhi ya matukio hayo yamekuwa yakichukuliwa hatua kali za kisheria.

Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Afrika Intiatives mkoani Shinyanga, akitoa mafunzo ya ufeminist kwa waandishi wa habari 15 ambao wapo kwenye Timu ya kuandika habari za kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mwandishi wa Habari Mwandamizi Kareny Masasy, akitoa mada kuhusu kalamu ya uandishi wa habari na ufeminist.
Mratibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga Estormine Henry akielezea namna utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa waandishi wa habari.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe Shabani Njia, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Mwandishi wa habari wa Radio Faraja Moshi Ndugulile akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Mwandishi wa habari wa ITV Frank Mshana akichangia mada kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye kazi ya vikundi kwenye mafunzo hayo.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.


TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807