Header Ads Widget

RAIS SAMIA; LUKUVI HATAGOMBEA USPIKA NA KAZI NAYE IKULU NA PARAMAGAMBA KABUDI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema aliyekuwa Waziri wa Ardhi William Lukuvi hatagombea Uspika wa Bunge bali amemsogeza Ikulu ili amsaidie kazi zake Ikulu huku Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi naye akipewa kazi maalumu Ikulu.

"...Kaka zangu Lukuvi na Kabudi, Hawa kiumri tunalingana. Sijawajumuisha katika baraza jipya kwa sababu nimeona niwalete karibu yangu tufanye kazi ya kuwasimamia nyie vijana.
Kabudi huyu atakuwa bosi wa mikataba ya uwekezaji, amefanya negotiations nyingi na sasa nimeona awe baba wa mikataba yote ya uwekezaji, baba wa negotiation zote.


Lukuvi mshamzulia maneno, mara anataka kugombea uspika, mara afadhali oooh alipoondolewa. Amefanya kazi kubwa sana, tuache kumchafua, nitakuwa naye Ikulu kwa kazi maalum ambayo itatangazwa baadaye", amesema Rais Samia.


"Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi. Hatagombania Uspika", amesema Rais Samia


"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba", ameeeleza Rais Samia

Post a Comment

0 Comments