Header Ads Widget

ASKARI UWANJA WA NDEGE KIA WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA, KUDHIBITI MADAWA YA KULEVYA

Mwandishi wetu, Kilimanjaro

ASKARI uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimamjaro (KIA),wametakiwa kutoa huduma bora kwa watumiaji wa uwanja huo, ambao ni lango kubwa la utalii, pamoja na kudhibiti uingizwaji wa madawa ya kulevya.

Kamanda wa Polisi wa viwanja vya ndege nchini, Jeremiah Shilla, ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea uwanja huo na kuzungumza na askari wa kituo kidogo cha Polisi KIA na kukagua makazi yao.

Amesema askari wa KIA wanapaswa kushirikiana na vyombo vingine kutoa huduma bora wakiwamo watalii wanaotumia uwanja huo.

Aidha, Kamishna Shilla  ameagiza Askari katika uwanja huo wa ndege wa kimataifa kilimanjaro(KIA), kudhibiti pia uingizwaji wa madawa za kulevya kwenye uwanjani hapo.

Amesema nilazima polisi waongeze bidii katika kukabiliana na madawa yakulevya katika uwanja huo, kwani bado kuna madawa mitaani.

Awali Mkuu wa kituo kidogo cha polisi KIA, Edith Makweli amesema polisi KIA wanafanyakazi vizuri.

Amesema kwa kushirikiana na vyombovingine wameweza kudhibiti uhalifu katika uwanja huo ikiwepo dawa za kulevya.

Kamanda Shilla kesho anatarajiwa kuzungumza na wanaotoa huduma za usafiri katika uwanja huo,kutembelea KIA na kuzungumza na wadau wa uwanja huo.

Askari wakiwa kwenye Gwaride.
Askari wakiwa kwenye Gwaride.
Askari wakiwa kwenye Gwaride.

Post a Comment

0 Comments