Header Ads Widget

ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA MICHEZO AZAM TV, AHMED ALLY ATEULIWA KUWA AFISA HABARI SIMBA SC


Aliyekuwa Mtangazaji wa Azam TV Ahmed Ally leo Jumatatu Januari 3,2022 ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano (Afisa Habari) katika Klabu ya Simba SC.

Kabla ya kutangazwa kuwa Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alikuwa mtangazaji wa Azam TV, lakini kabla ya hapo aliwahi kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye kampuni ya Sahara Media (Radio Free Africa na Star TV).

Kupitia ukurasa wa Facebook wa Simba SC wameandika:
"Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.


Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano. #NguvuMoja

Post a Comment

0 Comments