Header Ads Widget

WANAHABARI SHINYANGA WANOLEWA SHERIA ZA HABARI

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti, akizungumza kwenye mafunzo ya Sheria za habari kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

TAASISI ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN), imetoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Shinyanga, juu ya sheria ambazo zinagusa Tasnia ya habari, ili kuwaongezea weledi katika taaluma yao, na kuepuka kuingia kwenye adhabu za ukweukwaji wa sheria hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa MISA-TAN Andrew Marawiti, akizungumza leo Decemba 20/2021 wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, amesema waandishi wa habari wanapaswa kuzijua sheria na kuziishi ambazo zinagusa Tasnia yao, pamoja na kuzipigia kelele zile ambazo zina minya uhuru wa habari.

Alisema, Taasisi hiyo imekuwa ikiendesha mradi wa miaka miwili juu ya utoaji wa elimu za sheria za habari kwa wanahabari hapa nchini, kwa kushirikiana wa Taasisi ya International Media Support (IMS), ili kuongeza uelewa wa kuzifahamu sheria hizo na mapungufu yaliyopo, ambayo yanapaswa kufanyiwa maboresho ili kutoa uhuru wa habari.

“Sheria ambazo zinagusa Tasnia ya habari tutakazofundisha hapa Shinyanga kwa waandishi wa habari, ni Sheria ya huduma za habari (2016), Takwimu (2019), na Sheria ya udhibiti wa mawasiliano ya kielekitroniki na Posta (EPOCA) 2010,”alisema Marawiti.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Jesse Kwayu ambaye ni Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain, alisema waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini na sheria ambazo zinagusa Tasnia hiyo, sababu baadhi ya vifungu zinawabana katika utekelezaji wa majukumu yao na kunyimwa uhuru wa kupata au kutoa taarifa.

Aidha, alisema Serikali inapaswa kuzifanyiwa marekebisho sheria ambazo zinagusa Tasnia ya habari, kwa kurekebisha baadhi ya vifungu ambavyo vina minya uhuru wa habari, ili ziwe rafiki kwa ustawi wa nchi.

Nao baadhi ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga ambao wamehudhulia mafunzo hayo, walisema elimu hiyo ya sheria zinazogusa Tasnia ya habari, zitawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao na kuepuka kuingia kwenye matatizo. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) Andrew Marawiti, akizungumza kwenye mafunzo ya Sheria za habari kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga. Mwezeshaji wa mafunzo hayo Jesse Kwayu ambaye ni Mhariri Mwandamizi kutoka Kampuni ya Media Brain, akitoa mafunzo ya sheria za habari kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya sheria za habari.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments