Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI SHINYANGA WAKEMEA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA, WALAANI BIASHARA YA KUJIUZA KWA WATOTO WADOGO HASA MAENEO YA RELINI


Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk, Emmanuel Makala, akizungumza kwenye kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

VIONGOZI wa dini kutoka Madhehebu mbalimbali mkoani Shinyanga, wamekemea matukio ya ukatili wa kijinsia kuendelea kuwepo mkoani humo, huku wakiitaka Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria watu ambao bado wanaendekeza vitendo hivyo.

Wamebainisha hayo leo decemba 10,2021 wakati wa Kongamano la viongozi wa Dini na Jamii, la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, lililoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya Ziwa Victoria mkoani Shinyanga.

Walisema vitendo vya ukatili wa kijinsia vinaitia laana nchi na hata kusababisha mvua kutonyesha, na kuitaka jamii kuachana na vitendo hivyo, ili kupata Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuitaka Serikali isiwafumbie macho watu ambao wanafanya ukatili, wakiwamo ambao wanawatumikisha watoto wa kike katika biashara ya kuuza ngono.

Sheikh Balilusa Hamisi ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga, anasema viongozi wa kidini wanapaswa kupinga kwa nguvu zote vitendo vya matukio ya ukatili wa kijinsia ili jamii ibaki salama, ambapo wakinyamaza wao dunia itakosa mtetezi.

“Mtu yoyote atakaeona tukio ovu mbele yake anapaswa kulizuia, kulikemea kwa nguvu zote, pamoja na kulichukia, na sisi viongozi wa dini tuna laani matukio ya ukatili kuendelea ndani ya jamii, na ukiona kiongozi hakemei tukio la ukatili basi ana udhaifu wa imani,”alisema Sheikh Hamisi.

Naye Sheikh Khalifan Ally kutoka Msikiti wa Istiqama mjini Shinyanga, alilaani vitendo vya watu kuwatumikisha watoto wa kike kufanya biashara ya kuuza ngono, huku wakilindwa na Mabaunsa hasa katika maeneo ya stesheni ya Reli mjini Shinyanga kwa kuwalipa Shilingi 2,000.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria mkoani Shinyanga Dk. Emmanuel Makala, amesema Kanisa hilo linachukizwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa mabinti.

Amesema Kanisa hilo kwa sasa linatekeleza mpango wake wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambao ulianza mwaka 2020 kwa kutoa elimu ya kujitambua, na afya ya uzazi kwa wasichana.

Pia, amesema mbali na utoaji wa elimu hiyo, wamekuwa wakiwawezesha wasichana wakiwamo waathirika wa mimba na ndoa za utotoni, na kuwapatia elimu ya ujasiriamali na ushonaji, ili kutimiza ndoto zao na kuendesha maisha yao.

Mratibu wa kudhibiti ukimwi mkoani Shinyanga Dk. Peter Mlacha, akizungumza kwenye Kongamano hilo, alisema biashara ya ngono ni moja ya sababu ambayo inachangia mkoani huo kuwa na kiwango cha juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 5.9 ambapo kitaifa ni 4.9.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo Beda Chamatata, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewataka viongozi wa dini, kuendelea kupaza sauti za kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani humo, huku Serikali nayo ikiwachukulia hatua kali watu ambao hutenda ukatili huo.

Alitaja Takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani humo, kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, yametokea 5,845 ,watu wazima waliofanyiwa ukatili 3,335 na watoto 2,510, ambapo wahanga wakubwa wa matukio hayo ni wanawake na watoto.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk, Emmanuel Makala, akizungumza kwenye kongamano hilo la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo Beda Chamatata, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizunguma kwenye Kongamano hilo.

Sheikh Balilusa Hamisi ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga, akizungumza kwenye Kongamano hilo.

Mchungaji Charles Lugembe ambaye ni msaidizi wa Askofu kutoka Kanisa la AICT, akizungumza kwenye Kongamano hilo.

Sheikh Khalifan Ally kutoka Msikiti wa Istiqama mjini Shinyanga, akizungumza kwenye Kongamano hilo.

Mratibu wa kudhibiti ukimwi mkoani Shinyanga Dk. Peter Mlacha, akizungumza kwenye Kongamano hilo.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akizungumza kwenye Kongamano hilo.

Mwenyekiti wa dawati la utetezi haki za binadamu kutoka Lyabukale wilayani Shinyanga Unice Magesa akizungumza kwenye Kongamano hilo namna wanvyopambana kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.

Mwenyekiti wa dawati la utetezi haki za binadamu kutoka Dutwa wilayani Bariadi mkoani Simiyu Yohana Mayenga, akitoa taarifa namna wanavyopambana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.

Viongozi wa kidini kutoka Madhehebu mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano hilo.

Viongozi wa kidini kutoka Madhehebu mbalimbali wakiwa kwenye Kongamano hilo.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Kongamano la kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia likiendelea.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.Post a Comment

0 Comments