Header Ads Widget

SHINYANGA WAELEZA MAFANIKO YA TASAF, KAYA 7,155 ZAONDOLEWA KWENYE MPANGO

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha TASAF

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga, imeendesha kikao cha kujadili mafaniko na changamoto za utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini (TASAF), kwa kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi 2021.

Kikao hicho kimefanyika leo Decemba 24, 2021, katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, ambacho kilihusisha wadau wa mpango huo, wakiwamo na Waratibu wa TASAF ngazi za Halmashauri.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, amesema Serikali ilianzisha mpango huo wa TASAF, kwa lengo la kupunguza hali ya umaskini kwa wananchi, ambao wale wanaishi maisha duni.

Amesema katika Mkoa wa Shinyanga utekelezaji wa mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya maskini, ulianza rasmi julai mwaka 2015, ambapo mpaka sasa 2021 wameweza kufanikiwa kubadilisha hali za maisha kiuchumi za walengwa wa mpango huo.

“Katika Mkoa wa Shinyanga mafanikio ambayo tumepata katika utekelezaji wa mpango wa TASAF wa kunusuru Kaya maskini, Kaya 24,600 zimejiunga na Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa, Kaya 22,411 zimeanzisha miradi ya kiuchumi, Kaya 4,119 zimeboresha makazi yao na kujenga nyumba za bati, na zingine kula milo mitatu kwa siku,”amesema Omary.

Aidha, amewataka waratibu wa mfuko wa Bima ya Afya CHF, kulishughulikia tatizo la walengwa wa TASAF, ambao wana Bima hizo pamoja na wananchi, kuwapatia huduma stahiki za matibabu wanapofika kwenye huduma za Afya, sababu kumekuwa na malalamiko ya wagonjwa wenye Kadi hizo kunyimwa Madawa, na kwenda kununua kwenye maduka ya watu binafsi, tofauti na wale ambao hutoa pesa taslimu ambapo hupewa madawa bila ya usumbufu.

Katika hatua nyingine, amesema kwa wale walengwa wa TASAF ambao vidole vyao havitambuliwi kwenye malipo kwa mfumo wa kielekitroniki, waendelee kulipwa kwa njia ya kawaida, wakati taratibu za kuwalipa kwa njia ya simu na benki zikiendelea kufanyika.

Akizungumzia changamoto za baadhi ya walengwa ambao hawana vitambulisho ya Taifa NIDA licha ya kujaza fomu za maombi husika, amewaomba TASAF makao makuu wawasiliane na mamlaka husika, ili walengwa hao wapate vitambulisho hivyo, na kuingiziwa malipo yao kwa njia ya kielekitroniki.

Pia amewataka Waratibu wa TASAF ngazi ya Halmashauri, kwa kushirikina na wawezeshaji kuwakumbusha walengwa kutimiza masharti ya mpango huo, pamoja na kuibua miradi yenye tija ili ipate kuwainua kiuchumi na kuondokana na umaskini, na siyo fedha hizo kuzifanyia Anasa.

Ameeleza pia katika utekelezaji wa mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini TASAF 111 awamu ya pili mkoani humo, kwa kipindi cha kuanzia (2020-2023), kuwa jumla ya Kaya 14,785 zimekidhi vigezo na kuingizwa kwenye mpango huo, ambapo Kaya 7,155 zilikosa sifa na kuondolewa.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, amewataka waratibu wa TASAF mkoani humo, wawe wanawasaidia walengwa wa mpango huo, kuwapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuibua miradi ya yenye tija ikiwamo ufugaji wa mifugo, kilimo, na upandaji miti na kuwatoa kwenye umaskini.

Nao baadhi ya waratibu wa TASAF ngazi ya Halmashauri akiwamo Octavina Kiwone wa Manispaa ya Shinyanga, walitaja baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili kwenye utekelezaji wa mpango huo, kuwa baadhi ya walengwa hawazitumii fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kuendelea kukabiliwa na hali ya umaskini.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha TASAF.

Mratibu wa TASAF Mkoa wa Shinyanga Dotto Maligisa akizungumza kwenye kikao cha kujadili mafanikio ya TASAF na changamoto zake.

Mratibu wa TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango wa TASAF kwenye kikao hicho.

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Happy Shayo, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa TASAF kwenye kikao hicho.

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Ushetu Denis Pius, akiwasilisha taarifa ya utekeleza wa Mpango wa TASAF kwenye kikao hicho.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha TASAF.

kikao cha TASAF kikiendelea.

kikao cha TASAF kikiendelea.

kikao cha TASAF kikiendelea.

kikao cha TASAF kikiendelea.

kikao cha TASAF kikiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa kwenye kikao hicho cha TASAF

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.Post a Comment

0 Comments