Header Ads Widget

REA KUKAMILISHA MRADI WA UMEME KWA VIJIJI 216 KWA KISHAPU, SHINYANGA DC NA KAHAMA

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Na Estomine Henry, SHINYANGA

Vijiji vipatavyo 216 vya wilaya za Kishapu, Shinyanga na Kahama kunufaika na mradi wa REA kabla ya desemba-2022 kwa mradi huo awamu ya tatu mzunguko wa pili wenye thamani ya Sh. bilioni 60 ili kufikisha umeme kwa wananchi wa maeneo hayo.

Hayo yameelezwa leo desemba 1, 2021 na Kaimu Mkurugenzi wa REA Elineema Mkumbo alipo kabidhi mikataba ya mradi wa REA kwa wilaya hizo, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika zoezi la kutambulisha mradi huo wa REA unaotajiwa kutekelezwa kwa wilaya ya Kahama, Kishapu na shinyanga.

Mkumbo alisema kuwa mradi huu umegawanyika katika mafungu mawili ambapo kiasi cha Tshs bilioni 21 kwa wilaya ya Kishapu na shinyanga na Tshs bilioni 39 imetengwa kwa wilaya ya Kahama.Mradi huu utalenga kufikia vijiji 216 vilivyokusudiwa katika mradi wa REA.

Kaimu Mkurugenzi wa REA alisema kuwa mradi huo utatekelezwa na wakandarasi wawili ambao ni Suma JKT atakayetekeza wilaya ya Kishapu na Shinyanga na Tontan Project Technology Co Ltd amepatiwa eneo la wilaya ya Kahama.

Mkumbo alisema kuwa Tanesco, wakandarasi na viongozi wa vijiji kwa maeneo yote ya mradi watajadiliana kwanza ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza na kutambua maeneo yenye vipaumbele zaidi.

“Tunawataka wananchi wasikate tamaa kwa kuwa awamu hii maeneo yasiyo na umeme yatafikiwa kwa bajeti iliyotengwa na serikali’ Alisema Mkumbo

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zuwena Omary alishukuru REA kuwa mradi huo kusaidia kuondoa changamoto za umeme kwa maeneo ya vijiji na alisema serikali itasimamia na kufatilia mradi huo na kutoa ushauri kwa maeneo yatakayo kuwa na mapungufu.

“Changamoto bado ziko kwa maeneo baadhi ya vijiji kutopitiwa na umeme kwa au umeme kuwepo eneo lisilo na mahitaji ya tija na lakini ni vema uwajibikaji uwepo kwa REA, Tanesco na wakandarasi husika kwa kupeana taarifa za maendeleo ya mradi kila wakati ili kuepusha mapungufu yanayoweza kushughulikiwa mapema”

Msimamizi wa mradi wa REA kutoka mkoani Shinyanga Mhandisi Antony Tarimo alisema kuwa vijiji 216 vitanufaika kwenye hatua za awali za mradi ila bado vijiji 30 vitasalia ambavyo haviko kwenye mradi na serikali imetamka vyote vipate kuna uwezekano wa kuwepo mabadiliko ya mradi vijiji vyote vipate

Mkurugenzi wa masoko kutoka kampuni ya Tontan Project Technology Co. Ltd Nasra Mwampashe alisema kuwa wamejipanga kwa nguvu, akili na vifaa katika kutekelezwa mradi huo kwa kahama kwa kuzingatia mikataba kikamilifu.


Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akionesha Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajia kunufaisha vijiji 216 mkoani Shinyanga kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 60.

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo akizungumza wakati akitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo akizungumza wakati akitambulisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kukabidhi Mikataba itakayotumiwa na Wakandarasi Kutekeleza Mradi huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Elineema Mkumbo akielezea namna walivyojipanga kutekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili mkoani Shinyanga.

Msimamizi wa Miradi ya REA - TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Anthony Tarimo akielezea namna vijiji 216 mkoani Shinyanga vitakavyonufaika na Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Ukandarasi ya Tontan Project Technology Co. Ltd, Nasra Mwampashe akielezea namna walivyojipanga kutekeleza kwa ufanisi na weledi mkubwa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili wilayani Kahama.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blogPost a Comment

0 Comments