Header Ads Widget

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY, NACONGO WAZIJENGEA UWEZO ASASI ZA KIRAIA JUU YA SHERIA ZA NGO, NA ULIPAJI KODI

Afisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Foundation For Civil Society Ofisi ndogo ya Dodoma (FCS) Nicholaus Mhozya, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Asasi za kiraia mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Foundation For Civil Society (FCS) kwa kushirikina na Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO), wameendesha mafunzo kwa Asasi za kiraia 50 mkoani Shinyanga, namna ya kuzijua Sheria za NGO na kuzitekeleza, pamoja na ulipaji kodi ya Serikali. 

 
Mafunzo hayo yamefanyika leo Mjini Shinyanga katika ukumbi wa mikutano Karena, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary.

Akizungumzia malengo ya mafunzo hayo Afisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Foundation For Civili Society Ofisi ndogo ya Dodoma Nicholaus Mhozya, amesema madhumuni ya mafunzo hayo, ni kuzijengea uwezo Asasi za kiraia, kuzijua Sheria za NGO, pamoja na namna ya kulipa kodi ya Serikali, ili wafanye kazi zao bila ya kubuguziwa.

“Shirika letu za Foundationi For Civil Society tunatoa Ruzuku kwa Asasi za kiraia pamoja na kuzijengea uwezo, na leo tupo hapa mkoani Shinyanga, kujengeana uwezo, kuwa na uwelewa wa pamoja katika majukumu yetu, kuzijua Sheria za NGO pamoja na masuala ya ulipaji kodi, sababu mashirika ya kiserikali kuna kodi ambazo zinatuhusu kuzilipa kwa Serikali,”alisema Mhozya.

“Pia tunatakiwa kuzijua Sheria za NGO ambazo zinatuongoza sisi wenyewe ili wakati wa utekelezaji wa kazi zite kusiwe na bughuza yoyote ile na ndiyo maana tupo hapa leo ili Taasisi zetu ziendeshwe kwa weledi na kufikia malengo ambayo tumejiwekea,”aliongeza.

Naye Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NACONGO) mkoani Shinyanga Mussa Ngangala, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa NGO, ambayo yatasaidia kuimarisha mashirika yao na kuendelea kutoa huduma kwa jamii.

Naye Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, ameyapongeza Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani humo kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya ndani ya jamii, na kuahidi Serikali kuendelea kuyapatia ushirikiano katika kuwahudumia wananchi.

Aidha, alisema katika mkoa huo kuna Asasi nyingi za kiraia ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali na kuziasa katika utekelezaji wa miradi hiyo washirikiane na Maofisa maendeleo ya jamii, ili miradi yao inapofika kikomo Serikali ipate kuindeleza na kuifanya jamii isirudi nyuma bali iendelee kuishi salama.

“Asasi za kiraia mnafanya kazi nzuri za kuisaidia jamii, ila naomba mshirikiane na Maofisa wetu wa maendeleo, ili kuwe na uendelezaji wa miradi hiyo pale nyie mnapofika kikomo, sababu wakati wa utekelezaji wa miradi yenu jamii inakuwa salama kabisa, lakini mkiacha tu wanarudi kulekule ikiwamo kuendekeza masuala ya Mila na desturi Kandamizi,”alisema Omary.

Katika hatua nyingine alizitaka Asasi hizo ka Kiraia ziwe zinawasilisha Mpango kazi wao wa miaka mitatu Serikali, ili waone namna ya kushirikiana nao katika utekelezaji wa shughuli zao ndani ya jamii, pamoja na kuwasilisha taarifa za kila Robo Mwaka.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Serikali Dodoma Denis Bashasha, amezitaka Asasi hizo zifuate sheria za NGO na kuzitekeleza ikiwamo ilipaji wa Ada kila mwaka ambayo ina ambatana na taarifa ya fedha iliyokaguliwa ili kutosumbuliwa na Serikali pamoja na kulipa faini.

Pia alisema wanapopata fedha kutoka kwa wafadhili wawe na mikataba na wanapofanya mabadiliko yoyote kwenye Mashirika yao wawe wanatoa taarifa kwa msajili wa mashirika hayo.

Akitoa mada ya ulipaji Kodi Afisa elimu kwa mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Shinyanga Justine Katiti, alisema Asasi za kiraia zinapaswa kuwa zinalipa kodi Serikalini kama walipa kodi wengine kupitia Michango ya wanachama, Misaada, zawadi, kodi ya pango, pamoja na vyanzo vyao vingine vya mapato.

“Kiwango cha ulipaji kodi kwa Asasi za kiraia ni asilimia 30 ya mapato yao kila mwaka, mara baada ya kutoa gharama za uendeshaji,” alisema Katiti.

“Kodi ndiyo chanzo kikubwa cha mapato Serikalini, hivyo naziomba Asasi za kiraia mlipe kodi kwa wakati, ili kuisaidia Serikali kupata fedha za kuendesha shughuli zake mbalimbali,”aliongeza.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwamo Mathias Chidama kutoka Shirika la CHIDEP, wamesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa kwao ambayo yatakuwa chachu katika shughuli zao za kuhudumia jamii.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo ya Asasi za kiraia mkoani Shinyanga.

Kaimu Afisa maendeleo ya jamii mkoani Shinyanga Nyanjula Kiyenze akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Foundation For Civili Society Ofisi ndogo ya Dodoma (FCS) Nicholaus Mhozya, akielezea madhumuni ya mafunzo hayo ya Asasi za kiraia mkoani Shinyanga.

Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NACONGO) mkoani Shinyanga Mussa Ngangala, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NACONGO) mkoani Shinyanga Mussa Ngangala, akielezea umuhimu wa mafunzo hayo kwa Asasi za kiraia.

Afisa elimu kwa mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Shinyanga Justine Katiti, akitoa elimu ya mlipa kodi kwa Asasi hizo za kiraia.

Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Serikali Dodoma Denis Bashasha, akitoa elimu ya Sheria za NGO.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary (katikati) akisikiliza malengo ya mafunzo hayo ya Asasi za kiraia mkoani Shinyanga.

Washiriki wakiendelea na mafunzo.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea, (kulia) ni Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga Boniphance Chambi, akiwa kwenye mafunzo hayo ya Asasi za kiraia.


Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo. 

Na Marco Maduhu- SHINYANGA

Post a Comment

0 Comments