Header Ads Widget

KATAMBI AUNGURUMA SHINYANGA, AFUNGUKA MAMBO AMBAYO AMETEKELEZA JIMBONI KWAKE NDANI YA MWAKA MMOJA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ameendesha mkutano wa dhadhara wa kueleza mambo ambayo ameyatekeleza ndani ya mwaka mmoja wa ubunge wake, pamoja kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, amefanya mkutano huo wa hadhara, katika mtaa wa Majengo Kata ya Kambarage, akiwa ameambatana na wataalam, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Meya, pamoja na Kamati ya siasa ya CCM wilaya.

Akielezea mafanikio ambayo ameyafanya kwenye Sekta ya Afya, kuwa huduma zimeboresha kuwa karibu na wananchi, ikiwamo ujenzi wa Zahanati, vituo vya Afya, upatikanaji wa madawa pamoja na vifaa tiba.

Alisema pia katika Hospital mpya ya Rufaa ambayo inajengwa katika eneo la mwawaza, kunajengwa hospitali ya magonjwa ya mlipuko (Medical Tourism), ambayo itakuwa ikitibu magonjwa hayo ukiwamo ugonjwa wa UVIKO-19 ambapo kwa sasa ujenzi huo upo hatua ya msingi.

Kwa upande wa Sekta ya elimu, amesema alitoa kiasi cha fedha Sh.milioni 34.2 fedha za mfuko wa jimbo, kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa vyumba vya Madarasa, ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi.

Pia, amesema miundombinu ya barabara imeboreshwa katika maeneo mengi ya Manispaa ya Shinyanga, yakiwamo yale ambayo ni korofi, pamoja na kujenga madaraja na makaravati.

"Sasa hivi ndugu zangu wana Shinyanga ni kipindi cha kazi tu na siyo porojo, na nitaendelea kuchapakazi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo," alisema Katambi.

"Tumpongeze pia Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, ikiwamo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, miundombinu ya barabara, madaraja, na vituo vya afya," aliongeza.

Aidha, alisema kwa upande wa ardhi, tayari wameshapata fedha Sh.bilioni moja, kwa ajili ya kupima, urathimishaji, na uthamini wa maeneo, ili wananchi wapate hatimiliki na kwenda kuzitumia katika mambo mbalimbali ya kiuchumi.

Katika hatua nyingine ,amezungumza masuala ya kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ukiwamo ujenzi wa stendi kuu ya mabasi, Soko, maegesho ya malori, na ujenzi wa chuo kikuu ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha ((2022-2023) miradi hiyo itaanza kutekelezwa.

Pia amehidi wananchi wa jimbo hilo, kuendelea kutatua changamoto zao mbalimbali, likiwamo suala la umeme, maji, barabara, katika maeneo ambayo bado yana changamoto hizo.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, pamoja na Meya wa Manispaa hiyo Elias Masumbuko, kwa nyakati tofauti wakizungumza kwenye mkutano huo, wameahidi kuendelea kushirikiana na Mbunge Katambi, kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
 
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.
Diwani wa Kambarage Hassani Mwendapole, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Rafael Nyandi, akizunguzma kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusup Katopola, akijibu Maswali ya wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara.

Meneja wa TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Pamphil, akijibu Maswali ya wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Wataalam na viongozi wa Taasisi za Serikali wakiwa kwenye mkutano wa Mbunge Katambi.

Awali Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana na Ajira, akiwasili kwenye mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.Post a Comment

0 Comments