Header Ads Widget

ANWANI ZA MAKAZI KUTUMIKA KUPANGA MIPANGO YA MAENDELEO TANZANIA

  
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kamisaa wa Sensa ya watu na makazi Mhe.Anne Makinda akibonyeza kitufe kuzindua matumizi ya mfumo wa anwani za makazi jana Jijini Mwanza.Kulia kwake ni Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Ashatu kijaji na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Robert GabrielSpika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kamisaa wa Sensa ya watu na makazi Mhe.Anne Makinda akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mha.Robert Gabriel kibao chenye anwani za makazi  katika uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi jana jijini MwanzaSpika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kamisaa wa Sensa ya watu na makazi Mhe.Anne Makinda akimkabidhi Mkuu wa WIlaya ya Nyamagana Bi.Amina Makilagi kibao chenya anwani za makazi jana katika uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi jijini Mwanza

 

Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza wakiwa katika viwanja vya Shule ya Msingi Buhongwa kwa ajili ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi.

Na Daudi Manongi, WHMTH, Mwanza

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne Makinda amesema Mfumo wa anwani za makazi utaisaidia Serikali kupanga mipango ya Maendeleo, kuimarisha usalama, kuongeza ajira na Mapato ya Serikali.

Mhe. Makinda ameyasema hayo leo wakati akizindua mfumo huo katika viwanja vya shule ya msingi Buhongwa B kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.

“Nazipongeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadau wote kwa ushirikiano wao na jitihada walizoweka ili kuhakikisha mfumo wa anwani za makazi unatekelezwa katika nchi nzima”, amesema

Aidha, amesema mfumo huo utaendana na programu tumizi (mobile application) ya mfumo wa anwani za makazi ambayo itakayorahisisha matumizi na utekelezaji wa mfumo kwa kuzingatia kwamba itatumika katika kukusanya taarifa za Barabara, wakazi, makazi pamoja na kutoa anwani za makazi ya wananchi,kaya, ofisi na eneo la biashara.

“NImeelezwa kwamba programu tumizi imetengenezwa na wazawa,nitumie fuarsa hii kuwapongeza wataalamu wetu walioshiriki kuunda programu hii,hongereni sana vijana wetu,hili ni jambo la kujivunia sana kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha wanatumika katika kuleta maendeleo ya taifa letu” ameongeza.

Kwa upande mwingine Mhe. Makinda amesema kwa kutumia utaratibu huu wa anwani za makazi, mpango shirikishi ulioandaliwa baina ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar  wa kutekeleza zoezi hili utasaidia  sensa ya watu na makazi ya  mwakani kufanyika  vizuri sana kwa sababu pia itaonyesha wananchi wanapokaa na wanafanya kazi gani.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema mfumo huu wa anwani za makati ni mfuo mama wa mifumo mingi ya utambuzi.

Watanzania wamekuwa wakilalamika kuwa na mifumo mingi midogo midogo ambao inayowataka kujisajili na hivyo mfumo huu tumeweza kuunganisha na mifumo mingine kama ya afya, NIDA, mfumo wa Mamlka ya Mapato Tanzania kwenye TIN namba, kusajili makampuni BRELA na mfumo wa usimamizi wa viwanja.

Kama Wizara inayosimamia mifumo yote ya Mawasiliano tumekuja na mfumo huu ili turahisishe maisha ya watanzania kwenye kuyaendea maendeleo ya mapinduzi ya nne ya viwanda, lengo kuu ni kuondoa usumbufu na malalamiko ya watanzania”, amesema.

Ameongeza kuwa mwaka huu ni dhamira ya Wizara kila mwananchi anakuwa na anwani yake ya makazi katika eneo analoishi, eneo la ajira au eneo la biashara.

Aidha, ametoa wito kwa watendaji, viongozi na wataalamu hususani wa kata na mitaa kujengewa uwezo wa kutosha ili waweze kuwa na uelewa wa pamoja,waweze kuratibu, kusimamia na kutekeleza mfumo huu.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula amesema katika utekelezaji wa mfumo huu wa anwani za makazi Wizara yake ni mdau mkubwa katika kuandaa ramani za kidijitali ambazo zinatumika kama ramami za msingi katika utekelezaji wa anwani za makazi

Bila kuwa na anwani hizi za kidijitali utekelezaji wake unaweza usiwe rahisi sana kwa sababu tunawatambua watu wetu na maeneo yao kwa kufuata mfumo huu nitoe taarifa kuwa ni halmashauri tisa ziko tayari ambazo maandalizi ya ramani husika yamekamilika, amesema

Naye Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amesema hadi kukamilika kwa mradi huo kwa upande wa Halmshauri ya Wilaya ya Nyamagana mradi huo  huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni moja milioni mia sita hamsini na tano fedha ambazo kwa kiasi kikubwa ziilitolewa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 Hivi karibuni wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati akizindua mkakati wa  uelimishaji wa pensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma alisema licha ya uwepo wa tozo za makazi lakini lengo la Serikali ni kujua anunani za makazi, idadi ya makazi na aina ya nyumba zilizopo.

Mwisho.


 

Post a Comment

0 Comments