Header Ads Widget

WANAHABARI WAMETAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO KUELIMISHA JAMII KUACHANA NA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAANDISHI wa habari hapa nchini, wametakiwa kutumia kalamu zao kuelimisha jamii, kuachana na matukio ya ukatili wa kijinsia.
 
Hayo yamebainishwa leo na Mkufunzi Mwandamizi wa waandishi wa habari Alakok Mayombo kutoka Internews, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari, juu ya kuandika habari za kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia, katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili huo, mafunzo ambayo yamefanyika kwa njia ya mtandao zoom.

Alisema waandishi wa habari kwa kutumia Kalamu zao, wanauwezo mkubwa wa kuibadilisha jamii, kuachana na matukio hayo ya ukatili wa kijinsia.

"Waandishi wa habari mnauwezo mkubwa sana kuibadilisha jamii kuachana na matukio ya ukatili wa kijinsia kupitia Kalamu zenu, na hata kuondoa masuala ya mila na desturi Kandamizi," alisema Mayombo.

Naye Musa Juma, ambaye ni mwezeshaji wa mafunzo hayo, aliwasisitiza waandishi wa habari, katika kuandika habari za matukio ya ukatili wa kijinsia wazingatie usawa katika habari zao.

Kwa upande wake Ali Sultani, akitoa mafunzo hayo, amewakumbusha wanahabari, kuwa wanapokuwa wakitaka kuandika habari lazima wawe na wazo, na kujua nini wanacho lenga katika habari hiyo, pamoja na kufuata kanuni na maadili ya uandishi wa habari.

Nao baadhi ya waandishi wa habari ambao wameshiriki mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Internews, kwa nyakati tofauti walisema watayatumie vyema katika kuhabarisha umma, juu ya kuachana na matukio hayo ya ukatili wa kijinsia.

Post a Comment

0 Comments