Wakazi wa Manispaa na Mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kupata huduma za Matibabu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, huduma iliyokuwa ikitolewa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo kwa muda wa siku mbili.
Mratibu
wa huduma za lishe hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga ambaye pia ni mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza
Mkoa,na Mwenyekiti wa Chama Cha Magonjwa yasiyoambukiza Kanda ya Ziwa Bi. Lucy Kanoni
amesema kuwa jamii ya Mkoa huo na kanda ya ziwa haina utaratibu wa kupima afya mara kwa mara, hivyo hujikuta wamefikia hatua mbaya
zaidi za ugonjwa ikiwemo Sukari,
Shinikizo la damu na Moyo.
Lucy amesema
kuwa wameamua kutoa elimu ili waelewe magonjwa hayo na kuwawezesha
kuchukua tahadhari pamoja na kufanya vipimo kwa wnanachi mbalimbali ili kubaini
viashiria vya magonjwa na kuchukua tahadhari zaidi.
“Jukumu
letu ni kuhakikisha, tunatoa elimu ya kutosha kwa umma juu ya magonjwa haya
yasiyo ya kuambukiza ili wananchi wachukue hatua za kujilinda na kujikinga dhdi yake alisema Bi Lucy Kanoni.”
Lucy ameongeza kwa kusema kuwa lengo la hospitali na Mkoa ni kuona mwananchi yeyote haingii kwenye magonjwa hayo sababu akiingia huko si rahisi kutoka, hivyo jamii inapswa kubadilika ikiwemo mwenendo.
“Magonjwa haya ni hatari sana mfano Presha,Moyo na Mishipa ya damu, Kishukari na baadhi ya Kansa, Pumu, Figo na Selimundu(Sicocell) ambapo tunapomubaini mtu kuwa amepatwa na magonjwa haya huwa tunawaanzishaia huduma na matibabu Alisema Lucy ."
Katika
hatua nyingine Lucy amesema kuwa Moa wa Shinyanga umeendelea kuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaotokana na Magonjwa yasiyoambukiza ambapo kwa wiki moja wagonjwa wa
presha na moyo wapatao 10 ubainik.
“Kliniki zetu huwa tunafanya siku ya Jumanne tu kwa wiki moja, lakini uwa tunakuwa na wagonjwa
wengi sana hivyo huwa tunakuwa na wagonjwa wapatao 60 hadi 80 ambao wanakuja kliniki na kwa upande wa sukari kila wiki tunapata wagonjwa wanne, hii inatokana na Magonjwa haya kutokuwa
na dalili za wazi ambazo mgonjwa anaweza kuona na kuelewa haraka"Alisema Lucy .
Katika hatua nyingine Lucy
ameeleza, kuwa mitindo ya Maisha ambayo watu wanaishi kwa sasa ndiyo unachangia
watu wengi kukutwa na magonjwa hayo ambapo amezitaja baadhi ya sababu
zinazochangia magonjwa ya sukari moyo
ikiwemo ulaji usiozingatia utaratibu, kutofanya mazoezi,matumizi ya tumbaku na
matumizi makubwa ya pombe.
Kwa
upande wake Muuguzi katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Shinyaga ambaye ni miongoni
mwa watoa huduma waliokuwa wakitoa huduma kwa wananchi mbalimbali Bi Christina Jacob Kulima amesema kuwa zoezi hilo
limekwenda vizuri na zaidi ya wakazi 110 wamefikiwa na huduma hiyo kwa muda
wa siku mbili ambazo walikuwa wakitoa huduma na kupatiwa vipimo pamoja na Ushauri na Nasaha
Hata
hivyo Christina amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na wizara ya afya
mwaka 2012 zilibainisha kuwa katika watu 100 wenye umri wa miaka 25 na kuendelea watu 9 wana kisukari,
watu 26 wana shinikizo la juu la damu na watu 25 wana mafuta mengi kwenye damu huku 34 wakiwa na uzito uliopitiliza.
Selemani Omary ni mkazi wa Ibinzamata ameishukuru hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa kutoa huduma ya vipimo vya magonjwa yasiyoambukiza bure kwa wananchi na kuwataka vijana na makundi mengine kujenga tabia ya kupima mara kwa mara ili kubaini afya zao hali itakaowasaidia kuchukua tahadhari mapema
Omary ameongeza kuwa jamii kubwa ya kitanzania haina utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara hali inayochangia kukumbwa na magonjwa hayo ambayo huwa hayaonyeshi dalili zake mapema.
Naye Bi Nemetua Petro Mkazi wa Ngokolo ameishukuru hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa kutoa huduma bure kwa wananchi kwa kuwa wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Tazama Picha katika Matukio.
0 Comments