Header Ads Widget

MEYA AMPONGEZA DIWANI UJENZI OFISI YA CCM


Meya Mteule wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa kuwania Umeya Manispaa ya Shinyanga, kwa kupigiwa kura na Madiwani, na anasubiri kuapishwa (watatu kulia) akishiriki kwenye zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe jengo la Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Kata ya Ndala, (wapili kushoto) ni Diwani wa Ndala Zamda Shabani, pamoja na wana- CCM.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MEYA mteule wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa kuwania Umeya Manispaa ya Shinyanga, mara baada ya kupigiwa kura nyingi na Madiwani, ambapo kwa sasa anasubiri kuapishwa, amempongeza Diwani wa Ndala Zamda Shabani, kwa kujitoa kuanzisha ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Kata hiyo.
 
Ametoa pongezi hizo leo, alipowasili kwenye ujenzi wa Jengo hilo kushiriki na wanachama wa CCM, kuweka changalawe ndani ya msingi ili kuendeleza ujenzi wa Ofisi Chama, ambayo inatarajiwa kukamilika mwakani kwa gharama ya zaidi ya Sh. milioni 60.

Amesema kitendo alichokifanya diwani huyo, ni jambo jema ambalo linapaswa kuigwa na Madiwani wote Manispaa ya Shinyanga, ambao katika maeneo yao hakuna Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM.

“Nampongeza Sana diwani wa Kata hii ya Ndala Zamda Shabani, kwa kujitoa kuanzisha Jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, na mimi nina ahidi kumuunga Mkono pale atakapokwama ili kuhakikisha Ofisi hii inakamalika kwa wakati,”alisema Masumbuko.

Kwa upande wake diwani huyo Zamda Shabani, alisema alipoingia kwenye udiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, alisema moja ya ahadi yake katika kukisaidia chama, ni kujenga Ofisi ya Chama, ili waache kufanya vikao vyao chini ya miti.

Anasema alipotaka kuanzisha ujenzi wa Ofisi hiyo June mwaka huu, aliwasilisha wazo lake ndani ya Chama na kumpatia baraka zote, na kuanza kufyatua matofali na kisha kuanza ujenzi wa msingi ambao umeshakamilika kujegwa, na sasa wanataka kupandisha Boma.

Aidha, alisema baada ya kumaliza kujenga Ofisi hiyo ya Chama, pia atahamia kwenye ujenzi wa Zahanati, ambapo kwa sasa wapo kwenye hatua ya ukamilishaji wa ulipaji fidia wa eneo, huku akitoa wito kwa wananchi wa Ndala washirikiane na Serikali kuchangia shughuli za maendeleo.

Kwa upande wao wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi CCM ngazi ya Matawi Ndala ‘A’ na ‘B’ Robert Subi na Kasimu Salum, kwa nyakati Tofauti walisema ujenzi wa Ofisi hiyo utawasaidia kutunza siri za vikao vyao, sababu wamekuwa wakifanyia vikao chini ya Miti na hata kwenye nyumba za watu, ambapo siri zao huvuja na kuanza kugombana wao wenyewe.

Aidha, walisema watashirikiana na diwani huyo kukamilisha ujenzi wa Ofisi hiyo kupitia kamati ya ujenzi ambayo wameshaiunda, kwa kuchangisha fedha kwa wanachama, kushiriki nguvu kazi, na hata kuendesha harambee, lengo likiwa ni kuunga juhudi za diwani huyo.


Meya Mteule wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa kuwania Umeya Manispaa ya Shinyanga, na anasubiri kuapishwa, akizungumza kwenye ujenzi wa Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala.

Diwani wa Ndala Manispaa ya Shinyanga Zamda Shabani, akielezea namna alivyo anzisha wazo la kujenga Ofisi ya CCM kwenye Kata hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Tawi la Ndala 'B' Robert Subi, akielezea Ofisi hiyo namna itakavyo kisaidia Chama hasa kwenye uendeshaji wa vikao vya Chama, na kumpongeza Diwani kwa wazo la kuanzisha ujenzi wa Ofisi hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Tawi la Ndala 'A' Kasimu Salum, akizungumzia ujenzi huo wa Ofisi ya Chama na faida zake.

Mtendaji wa Ndala Lucas Magandula, akizungumzia faida za Ofisi hizo za CCM, kwa viongozi wa Chama na Wanachama wa Chama hicho namna kitakavyo wasaidia katika shughuli zao za kukijenga chama.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake CCM (UWT) Kata ya Ndala Rose Robert, akizungumzia faida za ujenzi wa Ofisi hiyo ya Chama.

Meya Mteule wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa kuwania Umeya Manispaa ya Shinyanga, na anasubiri kuapishwa (watatu kulia) akishiriki kwenye zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe jengo la Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Kata ya Ndala, (wapili kushoto) ni Diwani wa Ndala Zamda Shabani, Pamoja na wana-CCM.

Zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala likiendelea.

Zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala likiendelea.

Zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala likiendelea.

Zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala likiendelea.

Zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala likiendelea.

Zoezi la ufukiaji Msingi kwa Changalawe kwenye Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala likiendelea.

Muonekano wa msingi Jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala.

Muonekano wa Matofali katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Ndala.

Muonekano wa Matofali katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Ndala.

Kokoto zikiwa kwenye eneo la ujenzi.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.
Post a Comment

0 Comments