Header Ads Widget

SHINYANGA WAENDESHA KIKAO CHA DHARURA KUKABILIANA NA MATUKIO YA MIMBA, NDOA ZA UTOTONI

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, akizungumza kwenye kikao cha dharura cha kujadili na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili ndani ya jamii zikiwamo mimba na ndoa za utotoni.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SERIKALI mkoani Shinyanga wameendesha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili hali ya matukio ya mimba na ndoa za utotoni mkoani humo, pamoja na kuweka mikakati ya kutokomeza matukio hayo.

 Kikao hicho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) mkoani Shinyanga, na kushirikisha wadau kutoka Mashirika mbalimbali ya kiraia mkoani humo, ambayo yanatekeleza miradi ya ulinzi wa mtoto, likiwamo na Jeshi la Polisi.

Afisa Maendeleo ya jamii Mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, amesema wameendesha kikao hicho cha dharura, kwa kukutanisha wadau hao kutoka Asasi za kiraia na Jeshi la Polisi, kujadili namna ya kukabiliana na matukio ya mimba na ndoa za utotoni, na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio hayo, ili watoto wabaki salama na kutimiza ndoto zao.

“Katika kupambana na matukio haya ya ukatili wa kijinsia zikiwamo mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga, tushirikiane NGO na Serikali kutokomeza matukio haya ndani ya jamii, ikiwamo kutoa elimu kwa jamii kuacha vitendo vya ukatili,”alisema Ngwale.

Naye Wakili wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Mashitaka mkoani Shinyanga Salome Mbughuni, akizungumza kwenye kikao hicho, ameyataka Mashirika hayo kutoa elimu kwa wazazi kuacha kuchukulia mimba za utotoni kama fursa za kitega uchumi, na hatimaye kuharibu ushahidi wa kesi hizo, mara baada ya kumalizana na watuhumiwa kwa kupeana mali au mifugo.

Ofisa ustawi wa jamii mkoani Shinyanga Lidya Kwesigabo, ametoa ushauri kwa mashirika hayo, kuwa waandike maandiko ya kuomba ufadhili wa kujenga nyumba salama, ambayo itatumika kuhifadhi wathirika wa mimba za utotoni hadi kesi ina kwisha, na kuacha kurudi nyumbani kwao, na kurubuniwa na wazazi wake na kumkana mtuhumiwa.

Kwa upande wa Mashirika hayo akiwamo Grory Mbia kutoka mfuko wa ruzuku wa wanawake Women Fund Tanzania (WFT), alitoa ushauri kwa Serikali, kuwa wawe wanafanya vikao vya namna hiyo kila robo, na kufanya tathimini ya matukio ya ukatili pamoja na kupeana mrejesho wa kesi za matukio hayo, kuliko kumaliza mwaka mzima bila kikao chochote.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, akizungumza kwenye kikao hicho.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando akizungumza kwenye kikao hicho.

Wakili wa Serikali Ofisi ya Taifa ya Mashitaka mkoani Shinyanga Salome Mbughuni, akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Shinyanga Lidya Kwesigabo, akizungumza kwenye kikao hicho.

Daktari kutoka Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga Dk. Machiya Shilinde, ambaye hua ana husika pia kuchunguza waathirika wa matukio ya ukatili akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Ruzuku wa mfuko wa wanawake Tanzania (WFT) Grory Mbia, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, akizungumza kwenye kikao hicho.

Sabrina Majikata kutoka Shirika la ICS akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Miradi kutoka Shirika la YWCA John Eddy akizungumza kwenye kikao hicho.

Wadau kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga, wakiwa kwenye kikao hicho.

Wadau kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga, wakiwa kwenye kikao hicho.

Wadau kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga, wakiwa kwenye kikao hicho.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.





Post a Comment

0 Comments