Header Ads Widget

RC MJEMA AKOSHWA KASI UJENZI VYUMBA MADARASA WILAYANI KAHAMA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mwalimu Nyerere iliyopo Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameendelea na ziara yake ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, ambapo kwa sasa yupo wilayani Kahama akitembelea Halmashauri zote Tatu za wilaya hiyo ili kuona hutua ilipofikia jenzi hizo.

Mjema amendelea na ziara hiyo leo wilayani Kahama, mara baada ya kumaliza kutembelea Manispaa ya Shinyanga, wilaya ya Shinyanga, na Kishapu, kuona huta za ujenzi wa vyumba vya madarasa, na kuonesha kufurahishwa na Kahama, ambapo majengo yake yapo kwenye hatua ya kuoandisha Maboma, ufungaji, Renta na upauaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Msalala, na Manispaa ya Kahama, amesema amefurahishwa na kazi ya ujenzi huo, ambapo utafanya wafikie malengo ya kukamilisha mapema kabla ya Decemba 15, huku akiahidiwa Majengo hayo atakabidhiwa Novemba sababu yatakuwa yameshakamilika kujengwa.

"Wilaya ya Kahama kasi yenu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ni nzuri sana nimeipenda, na muendelee na kasi hiyo hiyo, na kukabidhi madarasa Novemba 20 hadi 28 kama mlivyo niahidi," alisema Mjema.

"Nataka katika mkoa wa Shinyanga tuwe wa kwanza kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa," aliongeza Mjema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, alisema katika wilaya hiyo wamepokea fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa Sh.bilioni 5.5 ambapo wanajenga Madarasa 247, na yote yapo katika hatua nzuri za ukamilishaji.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mwalimu Nyerere iliyopo Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ,( kulia) akiendelea kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Mwalimu Nyerere iliyopo Msalala wilayani Kahama, ambavyo vipo usawa wa kufunga Renta, (kushoto) ni Mkuu wa Shule hiyo Kafuru Songora.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akishiriki kujenga vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Ntobo iliyopo Msalala Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akikagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Mpera Manispaa ya Kahama.

Muonekano wa Majengo ya vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Mpera Manispaa ya Kahama.

Muonekano wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Isagehe Manispaa ya Kahama.

Muonekano vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Samia Manispaa ya Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (katikati) akiwa ziarani Wilayani Kahama , kukagua ujenzi wa vyumba vya Madarasa, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga na (kulia) ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba.

Na Marco Maduhu- KAHAMA.











Post a Comment

0 Comments