Header Ads Widget

RC MJEMA AFANYA ZIARA YA KIMKAKATI SHINYANGA, ATAKA UBORA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe; Sophia Mjema, akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga , katika ujenzi wa kituo cha Afya OldShinyanga katika Kijiji cha Ihapa.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga  Mhe; Sophia Mjema, ameanza ziara yake ya kikazi mkoani hapa, kwa kuzungumza na watumishi wa umma, pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo Sekta ya Afya na Elimu.

Mjema ameanza ziara yake leo katika Manispaa ya Shinyanga, ambapo aliambatana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Mkurugenzi wa Manispa hiyo Jomaary Satura, wakuu wa idara, pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika ujenzi wa Zahanati ya Bushushu iliyopo Lubaga, pamoja na kituo cha Afya Olshinyanga kilichopo kijiji cha Ihapa, ametaka miradi hiyo itekelezwe kwa kiwango kinachotakiwa ili kuendana na thamani ya fedha halisi (Value For Money).

“Nimekagua na kuona utekelezaji wa miradi hii ya ujenzi wa Zahanati na Kituo cha Afya kwa kweli inaendelea vizuri na kutia moyo, ila nawasihi mafundi muitekeleze kwa kiwango chenye ubora zaidi ili majengo haya ya dumu kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa wananchi,”alisema Mjema.

“Tunampongeza Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kutuletea fedha Sh.milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hii ya Bushushu, pamoja na Sh. milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Oldshinyanga, kitendo ambacho kitaondoa adha ya wananchi kufuata huduma ya matibabu umbali mrefu,”aliongeza.

Pia, alisema katika mkoa wa Shinyanga Rais Samia ametoa jumla ya Sh, bilioni 26, fedha ambazo zitatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Aidha, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, amewataka wafanye kazi kwa kujituma, uaminifu, mshikamano, kutunza siri za Serikali, pamoja na kuepuka vitendo vya Rushwa, ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye Manispaa hiyo.

Katika hatua nyingine Mhe; Mjema, amewaita wawekezaji wa vyuo vikuu wakawekeze mkoani humo, ambapo kuna maeneo mengi yametengwa kwa ajili ya uwekezaji, pamoja wawekezaji wa kilimo cha zao Alizeti, ambapo kwa sasa wana mbegu ambazo hukomaa kwa muda mfupi ndani ya Miezi Minne.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye miradi hiyo, aliwapongeza wananchi kwa kujitoa kufanya nguvu kazi, ikiwamo kuchimba msingi na kuwataka wawe na moyo huo huo wa kupenda maendeleo.

Alisema katika ujenzi wa miradi mingi ya maendeleo wilayani humo wananchi wamekuwa mstari wa mbele kujitoa katika nguvu kazi, kitendo ambacho wanawapa moyo viongozi kuwatekelezea miradi mingi ya maendeleo na kutatua changamoto ambazo huwakabili.

Nao baadhi ya akina mama wa Ihapa Oldshinyanga akiwamo Maria Joseph, waliipongeza Serikali kwa kuwajengea kituo hicho cha Afya, ambacho kitawasaidia kupata huduma ya matibabu karibu hasa wakati wa kujifungua watoto, ambapo mara nyingi hulazimika kwenda kujifungua katika Hospitali ya Rufani mjini Shinyanga.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa ukaguzi wa ujenzi kituo cha Afya OldShinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Shinyanga kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akielezea utekekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto), akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Bushushu iliyopo Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Ukaguzi wa Zahanati ya Bushushu ukiendelea.

Ukaguzi maendeleo ujenzi wa kituo cha Afya OldShinyanga katika Kijiji cha Ihapa ukiendelea.

Ukaguzi maendeleo ujenzi wa kituo cha Afya OldShinyanga katika Kijiji cha Ihapa ukiendelea.

Muonekano wa ujenzi wa Kituo cha Afya OldShinyanga katika hatua ya msingi.
Akina mama wakishiriki nguvu kazi kujenga kituo cha Afya OldShinyanga.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akimwagilizia Matofali katika Mradi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ambayo yatatumika kujenga vyumba vya madarasa 44 katika Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiangalia ubora wa Matofali hayo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akimwagilizia Matofali hayo.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akimwagilia Matofali hayo.

Awali watumishi wa Halmashauri Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye kikao nba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.



















Post a Comment

0 Comments