Header Ads Widget

MEYA MPYA MANISPAA YA SHINYANGA ELIAS MASUMBUKO AAPISHWA RASMI,, DC MBONEKO AMPA UJUMBE MZITO

Meya Mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akila kiapo Rasmi cha kuwa Meya wa Manispaa hiyo.

Na; Marco Maduhu, SHINYANGA

MEYA mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ameapishwa Rasmi leo kuwa Meya wa Manispaa hiyo, mara baada ya kupigiwa kura za Ndiyo, na Madiwani ambao wanatoka kwenye chama kimoja cha Mapinduzi CCM.

Zoezi la kuapishwa Meya huyo limehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, chama, Taasisi, wafanyabiashara, pamoja na wananchi, ambapo mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Masumbuko akizungumza mara baada ya kuapishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Solomon Lwenge, ameomba ushirikiano kwa watumishi wa Serikali na Madiwani, ili wawahudumie wananchi wa Manispaa ya Shinyanga na kuwaletea maendeleo.

Alisema katika uongozi wake kwa nafasi hiyo ya Umeya, amedhamilia kuwaletea maendeleo wananchi wa Manispaa ya Shinyanga, pamoja na kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo, ili zitekeleze malengo yaliyokusudiwa.

“Utendaji kazi mzuri na kufikia malengo ya kutumia wananchi, lazima tuwe wamoja, na ndiyo maana ninaomba tufanye kazi kwa ushirikiano, watumishi wa Serikali pamoja na madiwani, ili tusukume gurudumu la maendeleo pamoja,”alisema Masumbuko.

“Pia ninaomba watumishi muwe na nidhamu, waadilifu, wawajibikaji, na wawazi, sababu bila kuwa na vitu hivi hatutaweza kuwatumikia wananchi vizuri, wala kufikia adhima ya kuwaleta maendeleo,”aliongeza.

Katika hatua nyingine, Masumbuko ameahidi kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, na kusimamia matumizi ya mapato hayo, huku akiwataka watumishi wa Serikali pamoja na madiwani kubuni vyanzo vipya ya mapato, ili zipatikane fedha za kuendesha Halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alisema anafahamu utendaji kazi wa Meya huyo, huku akimsihi asimamie kikamilifu fedha za Halmashauri za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kwenda kujionea miradi inavyotekelezwa field na siyo kupewa taarifa za kwenye makaratasi.

“Naomba fedha hizi za mapato ya ndani uzisimamie vizuri na zikatekeleze miradi ya maendeleo na zisiliwe (kufanyiwa ubadhilifu) tunakata maendeleo katika mji wetu huu wa Shinyanga,”alisema Mboneko.

“Nafahamu utendaji wako kazi limetoka Jembe, limeingia Jembe hivyo sina shaka na wewe, na kuomba uchape kazi na mimi nitakuunga mkono,” aliongeza.

Pia aliwataka watumishi wa Umma kila mmoja afanye kazi kwa nafasi yake wala kusiwe na kikwazo kwa wawekezaji, ambapo Serikali imeshapa eneo la Tanganyika Pekazi lililopo OldShinyanga ambalo litatumika kwenye masuala ya uwekezaji.

Aidha, uchaguzi wa Meya Manispaa ya Shinyanga, ulifanyika mara baada ya aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo David Nkulila, kufariki dunia Agost Mwaka huu kwa maradhi ya ugonjwa wa Moyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza mara baada ya kumalizka kwa zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza kwenye zoezi ka kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza kwenye zoezi la kuapishwa Meya Mpya wa Manispaa hiyo Elias Masumbuko.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akitangaza Matukio ya upigaji kura kumchangua Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, kuwa amepata Kura zote 20 za Ndiyo, na hakuna Hapana wala kura iliyoharibika.

Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza mara baada ya kumaliza kuapishwa kuwa Rasmi Meya wa Manispaa hiyo.

Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za Mtaa Manispaa ya Shinyanga Nassoro Warioba akizungumza kwenye zoezi la kuapishwa Meya Mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Solomon Lwenge, (kushoto) akimuapisha Meya Mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kulia).

Meya Mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kulia) akiapa kiapo cha Maadili kutoka kwa Katibu msaidizi Ofisi ya Rais Sekretariet ya Maadili ya uongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora Gerald Mwaitembe (kushoto).

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko,(kushoto) akimpatia Kitabu cha Kanuni za kudumu za Halmashauri, Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kulia).

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, (kushoto) akimpatia Ilani ya CCM, Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Viongozi wa dini wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Wananchi wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Ushuhudiaji zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko likiendelea.

Mawakili, watumishi wa Serikali Manispaa ya Shinyanga , wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye zoezi la kuapishwa Meya mpya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.

Madiwani wakifuarahi mara baada ya kutangazwa matokeo kuwa Elias Masumbuko, ambaye ni Diwani wa Chamaguha kuwa amepata kura zote za Ndiyo kuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Wananchi wa Chamaguha wakifuarahia Diwani wao Elias Masumbuko kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Wananchi wakiendelea kufurahia.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune awali akipiga kura ya Ndiyo kumpitisha Elias Masumbuko kuwa Meya mpya wa Manispaa hiyo.
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mkadamu, ambaye pia alishindwa Nafasi ya Umeya na Elias Masumbuko, akipiga kura ya Ndiyo kumpitisha Elias Masumbuko kuwa Rasmi Meya wa Manispaa hiyo.
Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri akipiga kura ya Ndiyo kumpitisha Elias Masumbuko kuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga Hassani Mwendapole, akipiga kura ya Ndiyo kumpitisha Elias Masumbuko kuwa Meya wa Manispaa hiyo.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA.


Post a Comment

0 Comments