Header Ads Widget

MCHUNGAJI KWILEMBA ATAKA WATANZANIA WOTE WAOKOKE, AKEMEA UTENDAJI MAOVU

Mchungaji Charles Kwilemba akimwabudu Mungu kwenye Ibada ya sifa

Na Suzy Luhende, SHINYANGA

MCHUNGAJI wa Kanisa la Philadelfia Miracle Temple lililoko Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Charles Kwilemba, amewataka Watanzania wote kuokoka, na kuacha kutenda mambo maovu, ili kudumisha amani na utulivu.

Ushauri huo ameutoa jana kwenye Ibada ya sifa ya kumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu, iliyofanyika katika Kanisa hilo, ambapo amesema watu wakiokoka na kumjua Mungu wataacha kutenda mambo maovu. ambapo  amani na utulivu utazidi kutawala, huku wakimsifu Mungu na kumuabudu katika roho na kweli.

"Watu wote tukiokoka katika roho na kweli Mungu atatubariki na kila tutakachokifanya na tutakachokiomba kitajibiwa kwa wakati, hivyo ni vizuri tukaishi katika wokovu huku tukimrudishia sifa na utukufu mwenyezi Mungu,"alisema Kwilemba.

Aidha Mchungaji Kwilemba alisema Mungu amefanya matendo makuu mengi ya ajabu kwa wanadamu, hivyo inawapasa kuokoka na kumwabudu siku zote, ili awatendee Mambo makubwa.

"Katika kitabu cha Zaburi 139:14 -15 Daudi alimshukuru Mungu kwa kusema, nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha, matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana, mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoumbwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi, hivyo na sisi hatuna budi kumsifu Mungu wetu"amesema Kwilemba.
Naye Mchungaji Anania Clementi, alisema watu wengi wanakata tamaa katika wokovu, wakizani kwamba Mungu amewaacha, na kusahau kwamba Mungu anajibu kwa wakati na kuwataka watu wote waendelee kumuomba ambapo ipo siku atatenda kwa wakati wake kwani hachelewi wala hawai.

Clementi alisema mkristo anatakiwa kumsifu Mungu na kumwabudu katika roho na kweli, kwa sababu anafurahishwa na wamsifuo katika roho na kweli, na kumwimbia nyimbo mpya kila wakati kwa kuwa anastahili.

Kwa upande wake Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Baraka Raizer, alisema Wakolosai 3:16 inasema Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni, huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Aidha Raizer aliwaomba Watanzania wote wamtegemee Mungu siku zote za maisha yao, ili waweze kuziteka Baraka alizowaandaliwa wana damu, na waache kumtegemea shetani kwa sababu vyote vilivyopo hapa duniani ni mali ya Mungu.


Waumini wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple wakimsifu Mungu na Kumwabudu katika ibada ya sifa na kuabudu iliyofanyika kanisani hapo.

Waumini wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple wakimsifu Mungu na Kumwabudu katika ibada ya sifa na kuabudu iliyofanyika kanisani hapo.

Na Suzy Luhende, SHINYANGA.


Post a Comment

0 Comments