Header Ads Widget

BARRICK NORTH MARA YAZINDUA PROGRAMU YA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYABIASHARA WA NDANI


Meneja Uhusiano wa Jamii wa Barrick North Mara,Gilbert Mworia akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela,Hassam Massala akiongea wakati wa uzinduzi wa Programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.
*******

Mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick umetaja makampuni 20 ambayo yatashiriki kwenye programu ya maendeleo ya kibiashara ambayo itakuwa inatekelezwa na kampuni ya Kengo Consulting na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). 

Makampuni hayo yameorodheshwa kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani wa uchimbaji madini kama vile ujenzi, mazingira na biashara ya kilimo. 

Lengo la programu hiyo ni kuimarisha uwezo wa biashara za ndani ili ziweze kunufaika na fursa zilizopo kwenye sekta ya madini. Aidha, sekta hii inatabiriwa kuchangia uchumi na kufikia pato la taifa la asimilia 10 kufikia mwaka 2025.

Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Barrick Mark, Bristow, alisema kuwa programu hii ni udhihirisho wa jitihada endelevu za Barrick katika kujenga uwezo wa watu wa ndani.

“Tangu mgodi uanze kufanya kazi, tumekuwa tukishirikiana na wakazi wa maeneo yanayozunguka mgodi wetu kwa kutengeneza fursa za uchumi endelevu kupitia mkakati wa usambazaji wa bidhaa za ndani kwa ajili ya uchumi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla,” alisema.

Lengo mahususi kwa jamii ni kuwekeza kwenye maendelevu endelevu kiuchumi, na programu hii ni itachangia kulitekeleza hilo.

“Programu hiyo ya maendeleo ya biashara za ndani italeta mabadiliko makubwa kwenye mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini na tunategemea uwezo wa makampuni yanayoshiriki kuweza kuimarika na kutumia fursa zilizopo kwenye mnyororo huo wa thamani,” alisema.

Serikali ya Tanzania iliunda sera ya maudhui ya ndani ya mwaka 2015 ikilenga sekta ya madini, mafuta na gesi ili kuhakikisha uchimbaji wa madini na mapato yake yanawanufaisha watanzania.

 Sera hiyo na kanuni zake inalenga kupanua uwanda wa kibiashara kwenye uchumi wa Tanzania, kutengeneza nafasi za ajira kwa kuhamasisha maendeleo ya taaluma na uwezo wa watanzania kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.
Wageni waalikwa na wafanyabiashara walengwa wakiwa katika uzinduzi wa Programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.
Wageni waalikwa na wafanyabiashara walengwa wakiwa katika uzinduzi wa Programu ya kuwaendeleza wafanyabiashara wa ndani katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments