Header Ads Widget

MARUFUKU YA WASICHANA WAJAWAZITO KURUDI SHULENI ILIVYOHARIBU MAISHA YAO TANZANIA


Marufuku ya Tanzania kwa wanafunzi na wasichana waliobaleghe wajawazito wanaohudhuria shule imewanyima makumi ya maelfu ya wasichana haki yao ya kupata elimu, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights watch limesema .
 
Shule za umma kote Tanzania Bara hufanya upimaji wa lazima wa ujauzito kwa wanafunzi wa kike na kuwafukuza wasichana wajawazito kabla ya kumaliza masomo yao .

Serikali ya Tanzania haijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo .Msemaji wa serikali Gerson Msigwa alielekeza BBC kuwasiliana na waziri wa Elimu profesa Joyce Ndalichako kuhusu suala hilo.

BBC inaendeleza juhudi za kupata tamko kutoka kwa waziri Ndalichako au wizara yake .

Tangu Juni 2017, Rais wa zamani hayati John Magufuli na mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alichukua madaraka mnamo Machi 2021, wametekeleza marufuku rasmi dhidi ya wanafunzi ambao ni wajawazito au ni akina mama.

"Wasichana wa Tanzania wanateseka kwa sababu serikali inatekeleza sera hii ambayo inamaliza elimu yao, inawadhalilisha na kuwatenga, na kuharibu maisha yao ya baadaye," alisema Elin Martinez, mtafiti mwandamizi wa haki za watoto katika shirika la Human Rights Watch. "Serikali inapaswa kuondoa haraka sera hii isiyo ya kibinadamu na kuruhusu wanafunzi wajawazito na mama kurudi shuleni."

Human Rights Watch mnamo Julai na Agosti iliwahoji wasichana na wanawake 30 wenye umri kati ya miaka 16 hadi 24. Wote walikuwa wamefukuzwa shuleni au wameacha kwenda shule ya msingi au sekondari kati ya 2013 na 2021 kwa sababu walikuwa na ujauzito.

Mnamo Juni mwaka huu Serikali ya Tanzania ilitangaza kuwaruhusu wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa kwasababu ya kupata mimba kurejea masomoni kupitia vyuo vya maendeleo ya wananchi

Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dk Leonard Akwilapo aliwataka wakuu wa vyuo vya maendeleo ya wananchi kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike walioshindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba wanarudi na kuendelea na masomo.

Aliwataka wakuu hao wa vyuo kutekeleza agizo hilo la kudahili wanafunzi hao kupitia mpango wa elimu ifikapo mwaka 2022.
 
SOMO HAPA ZAIDI CHANZO BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments