Header Ads Widget

MADAKTARI BINGWA BUGANDO WATOA MATIBABU KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFANI MKOANI SHINYANGA,, WATOA WITO KWA WANANCHI..


Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Rufani Kanda ya Bugando, wakitoa matibabu kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga.

Na Josephine Charles, SHINYANGA.

WANANCHI mkoani Shinyanga, wametakiwa kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara, kwa kuwa magonjwa mengi hasa ya ndani siyo rahisi kugundulika mapema, ili watakapogundulika wapate matibabu kwa haraka na kuokoa afya zao.

Hayo yamesemwa  leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani na Magonjwa ya Moyo kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dr. Andrew Luhanga, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Rufani  Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye zoezi la kutoa Huduma za afya kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali leo.

Dk. Luhanga amesema lengo la kutoa huduma hiyo waliyoita clinic Tembezi kwa mkoa wa Shinyanga, ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hospitali ya Bugando,hivyo wanatoa huduma ya matibabu kwa hospitali za rufaa za mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera,Geita Mara,Simiyu na Shinyanga ukiwa ni mkoa wa tano kufikiwa na clinic hiyo.

Amesema kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga mwitikio ni mkubwa, watu wamejitokeza si chini ya 360 tangu walivyoanza kutoa huduma hiyo jana na wanatarajia kupata wagonjwa wengi zaidi hadi hapo kesho wanavyoenda kuhitimisha huduma ya clinic tembezi kwa mkoa wa shinyanga.

Ameeleza wagonjwa waliojitokeza kwa wingi ni pamoja na wanaosumbuliwa na magonjwa ya ndani,moyo,afya ya akili,Upasuaji sanifu,magonjwa ya kina mama,upasuaji wa koo,masikio na pua.

Amefafanua zaidi kuwa magonjwa ya moyo hayana dalili za moja kwa moja lakini dalili zinazojitokeza ni zile ambazo mgonjwa amefikia hatua za mwishoni kama mtu kushindwa kupumua,miguu kuvimba na kama ni mtoto anashindwa kulia,hakui vizuri au kubadilika rangi kuwa wa blue.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu akiwemo Juliana Bukoye na Steven Kudililwa wote wakazi wa manispaa ya shinyanga wameshukuru kufikiwa na huduma ya clinic tembezi ila wameomba kuongezwa kwa siku ya huduma kwa kuwa watu ni wengi na wengine tangu jana hawajahudumiwa na pia wameomba wasiwe wanafika kipindi cha maadhimisho fulani badala yake wajiwekee utaratibu wa kutembelea hospital ya shinyanga nje ya maadhimisho.


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani na Magonjwa ya Moyo kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dr. Andrew Luhanga,,akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Madaktari Bingwa ya Bugando wakitoa matibabu kwa wagongwa katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga.

Awali wananchi wakiwa wamejitokeza kupata matibabu kutoka kwa Madaktari hao Bingwa.

Wananchi wakiendelea kupata vipimo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Post a Comment

0 Comments