Header Ads Widget

WANANCHI WAMPA TANO KATAMBI UJENZI DARAJA UZOGORE- BUGWANDEGE

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akiwa ameshika kitabu cha ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwenye mkutano wa hadhara Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, mara baada ya kutembelea ujenzi wa daraja la Uzogore- Bugwandege.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Wananchi wa vijiji vya Uzogore na Bugwandege Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, kwa kuwajengea daraja ambalo lina unganisha vijiji hivyo.

Wananchi wamebainisha hayo leo wakati Mbunge huyo ,alipofika kwenye daraja hilo kuangalia maendeleo ya ujenzi wake, ambalo lipo katika hatua nzuri ya ukamilishwaji, pamoja na kufanya mkutano wa hadhara wa kutatua kero zao.

Wamesema kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutawaondolea hofu ya kusombwa na maji kipindi cha mvua, ambapo maji yalikuwa yakijaa na kupita hivyo hivyo, huku baadhi ya wanafunzi wakikatisha masomo kwa muda.

"Tuna mshukuru Mbunge wetu Katambi kwa kutujengea daraja hili ambalo lina unganisha vijiji viwili vya Uzogore na Bugwandege, ambalo ni kiungo muhimu sana katika Shughuli za kiuchumi," amesema Emmanuel Martini.

"Pia daraja hili limetuondolea changamoto ya watoto kutokatisha vipindi tena vya masomo wakati wa mvua, kwa kuhofia kusombwa na maji," ameongeza.

Naye Diwani wa Ibadakuli Msabila Malale, amesema daraja hilo ni kiungo muhimu sana kwa maendeleo ya wananchi wa vijiji hivyo viwili, na kumpongeza Mbunge Katambi kwa kusikiliza kilio hicho cha wananchi.

Kwa upande wake Mbunge Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi, Vijana, na Ajira, Patrobas Katambi, amesema alipofanya ziara kwenye vijiji hivyo, alijionea mwenywe ubovu wa daraja hilo na kuamua kutafuta fedha za kulijenga.

Aidha amesema fedha za ujenzi wa daraja zilipatikana Sh.milioni 420 na sasa linaendelea kujengwa, na zimeshapatika fedha zingine kiasi cha Sh. milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa kingo.

Pia amewahidi wananchi hao wa Ibadakuli kuendelea kutatua changamoto zao ,ikiwamo ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Afya, Elimu, Maji, na Umeme.

Katika hatua nyingine amewataka Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kazi nzuri ambayo anaifanya ya kuwaletea maendeleo, na kuwapuuza wale ambao wanapinga kila kitu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, watatu kutoka kushoto, akikagua ujenzi wa miundombinu ya barabara inayounganisha vijiji vya Uzogore na Bugwandege Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akiendelea na ukaguzi wa miundombinu ya barabara inayo unganisha vijiji viwili vya Uzogore na Bugwandege.

Ukaguzi ujenzi wa daraja ukiendelea.

Ukaguzi ujenzi wa daraja ukiendelea.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akiwa ameshika ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM kwenye mkutano wa hadhara Ibadakuli, na kuwaeleza wananchi yale yote ambayo ana yatekeleza kwao yamo kwenye ilani hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akiwa ameshika kitabu chenye Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassani kwenye mkutano wa hadhara Ibadakuli.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobasi Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akizungumza na wananchi wa Ibadakuli kwenye mkutano wa hadhara.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga Msabila Malale, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.

Diwani wa Vitimaalum Zuhura Waziri akizungumza na wananchi wa Ibadakuli kwenye mkutano huo wa hadhara.

Wananchi wa Ibadakuli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi, ambaye pia ni Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments