Header Ads Widget

WILAYA YA SHINYANGA YATENGA SH. MILIONI 12 KUTEKELEZA AFUA ZA LISHE ILI KUPUNGUZA UDUMAVU NA UTAPIAMLO

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (katikati) akizungumza katika katika kikao cha kujadili utekelezaji wa afua za lishe wilayani humo. Kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Geoffrey Mwangulumbi na Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba

Na Shinyanga Press Club Blog
WILAYA ya Shinyanga kupitia halmashauri zake mbili za Manispaa ya Shinyanga na Shinyanga DC imetenga zaidi ya Sh. Milioni 12 kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe wilayani humo ili kusaidia kupunguza changamoto ya uwepo wa watoto wenye utapiamlo na udumavu.

Hayo yameelezwa Juni 11, 2021 mjini Shinyanga wakati wa kikao cha kujadili hatua za utekelezaji wa afua za lishe, ambapo maafisa lishe wa halmashauri hizo walitoa taarifa za utekelezaji huo katika kikao kilichowakutanisha watendaji wa kata, wahudumu wa afya ngazi ya jamii, wakurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili namna ya kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto wenye changamoto hizo.

Wakitoa taarifa za halimasahuri zao katika utekelezaji wa afua za lishe, Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Saidi Mankiligo ameeleza kuwa halmashauri hiyo imetenga zaidi ya Shilingi milioni 4 kwa ajili ya utekelezaji wa afua hizo, huku Joanitha Jovine akieleza kuwa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetenga jumla ya Shilingi milioni 8 kwa ajili ya kutekeleza afua hizo.

Kwa upande wake Katibu wa kikao hicho ambaye ni M Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Geoffrey Mwangulumbi amesema
 wao kama watendaji wameamua kutenga fedha hizo ili kuchochea na kutimiza azma ya serikali katika kuboresh afua za lishe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho amewaagiza watendaji wa kata wilayani humo kuhakikisha wanaacha tabia ya kukaa maofisini badala yake waende vijijini kwa wananchi kuhamasisha utekelezaji wa afua za lishe na kwamba kwa mtendaji yeyote atakaye shindwa kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (katikati) akizungumza wakati wa kikao hicho
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geoffrey Mwangulumbi (kushoto) akiwasilisha taarifa kwenye kikao hicho
Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Shinyanga, Sanya Antony (kushoto) na Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mameritha Basike (kulia) wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kikao hicho
Wajumbe wa afua za lishe wilayani Shinyanga wakiwa kwenye kikao kilichowakutanisha Juni 11, 2021 mjini Shinyanga





Post a Comment

0 Comments