Header Ads Widget

TRA MWANZA YAKUSANYA SH. BILIONI 171 MWAKA WA FEDHA 2020/2021

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga (Katikati) akizungumza na wafanyabiashara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)Mkoa wa Mwanza Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Julai mwaka jana hadi Mei mwaka huu ilipangiwa kukusanya Sh. bilioni 184.55 na ilifanikiwa kukusanya Sh. Bilioni 171.00 ambayo ni sawa na asilimia 93.

Hayo yalisema na Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Joseph Mtandika wakati akizungumza katika kikao cha utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango mahususi wa mamlaka hiyo na TCCIA pamoja na Wafanyabiashara.

Alisema lengo la kikao hicho nikukumbushana taratibu mbalimbali za kikodi kujadili na kutatua changamoto za wafanya Biashara na kupokea maoni kwaajili ya kuboresha zaidi.

"Mwezi huu tulionao kuanzia Juni Mosi hadi sasa tumekusanya Sh. BilionI 10.9 lakini lengo letu kwa Mwezi huu ni kukusanya bilion 18 hivyo natumia nafasi hii kuwaomba na kuwakumbusha wafanyabiashara na walipa kodi kwa ujumla kutimiza wajibu wao ili mwaka wa fedha unapoenda kuisha wawe hawana madeni ya nyuma," alisema.

"Jukumu la Mamlaka ya mapato ni kukusanya mapato ya serikali ili uchumi wa nchi uzidi kuimarika,niwajibu wetu kutoa elimu kwa walipa kodi na Watanzania kwa ujumla pamoja na kutoa huduma bora ili kuongezea lidhaa ya hiari ya ulipaji kodi na kupanua wigo wa upatikanaji wa mapato",alisema Mtandika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Dk. Elibariki Mmali alisema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kufanya maonyesho lengo ikiwa ni kuwaunganisha wafanya biashara wa Mwanza na nje ya mkoa.

"Maonyesho haya yamekuwa na faida kubwa sana, Wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza wamefanikiwa kupanua wigo wa bidhaa zao kwa kukutana na wafanyabiashara kutoka mikoa mingine, wawekezaji mbalimbali wanaokuja kununua malighafi na muda mwingine wanauza hapo hapo na kumaliza hivyo ni fursa kubwa katika nchi yetu", alisema Mmali.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga alisema kuwa ni vyema Wafanyabiashara wawe na utaratibu wa kulipa kodi bila kushurutishwa ili kuweza kuimarisha uchumi wa taifa letu.

"Taifa imara linatokana na uchumi imara hivyo kuweni wazalendo katika ulipaji wa kodi na kwakufanya hivyo itawasaidia kufanya kazi zenu kwa uhuru na amani", alisema Senyi.

Nao Wafanyabiashara walisema wanafurahishwa sana na jinsi wanavyoendelea kupewa elimu ya ulipaji wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania na tunaahidi kumaliza madeni yote tunayodaiwa kabla ya Juni 30, mwaka huu.
Wafanyabiashara wakiwa kwenye kikao katika ukumbi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoa wa Mwanza


Post a Comment

0 Comments